El Shadai.

<< uliopita

ijayo >>

  Siri hiyo ya Kristo.

Yehova-Yire #2.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Yehova-Yire #2.

Sasa tumekuwa tukiongea juu ya mtumishi Wako mtiifu, Abrahamu, tukiendelea naye jioni hii, katika safari yake. Tunaomba kuwa utatubariki tunapoendelea chini njiani mwa miaka mamia mengi iliyopita, tukiwa na mtumishi mwaminifu aliyeamini Neno Lako. Hebu hilo liwe mfano, kama Paulo alivyosema katika Waebrania, kwa kile Abrahamu alichokuwa, mfano. Na tunaomba kwamba yeye, ile imani yeye aliyokuwa nayo, itafunuliwa kwetu jioni hii; tuamini Neno la Mungu, na hapana shaka juu Yake, Neno moja la Hilo, bali tuliamini Hilo lote, na tuamini kila kitu Yeye alichosema. Na hebu sisi tuweze kushikilia hizo ahadi ambazo Yeye alifanya kwa ajili yetu, na tuwe watoto wa Abrahamu kwa kuwa ndani ya Kristo. Tunaomba hilo katika Jina la Yesu. Amina.

----
Abrahamu alikuwa na umri wa miaka tisini na tisa, na wakati wote huu kamwe hakuyumba, bali aliliamini Neno la Mungu; na kuita yale mambo yasiyokuwepo kama kwamba yalikuwepo, kwa sababu Mungu alisema hivyo, bado akiamini yule mtoto angekuja, akishikilia ile ahadi. Ni mtu aliyoje! Ni ndugu aliyoje! “Abrahamu, ambaye dhidi ya tumaini... Tumbo la uzazi la Sara lilikuwa limekufa. Abrahamu alikuwa tasa. Mwili wa Abrahamu ulikuwa umekufa. Biblia ilisema ulikuwa umekufa, kwamba mwili wake ulikuwa kama uliokufa. Na tumbo la uzazi la Sara lilikuwa limekufa. Na Sara sasa alikuwa amekaribia sana miaka arobaini tangu akome hali ya kike, na bado Abrahamu aliliamini hilo, kwamba Sara angelikuwa na yule mtoto kwa sababu Mungu alisema hivyo. Hilo ndilo jambo lenyewe. Akilishikilia Neno kwa sababu Mungu alisema hivyo! Haidhuru kitu gani, zile kanuni za imani za dini zilizolifunika Hilo, na bado hilo Neno lilikaa pale! Ilipasa hiyo ije. Na hilo Neno likiwa limekaa katika moyo wa Abrahamu!

Haidhuru ni miaka mingapi, “Siku za hili zimekwishakupita, na lile pale.” Maadam hilo Neno limekaa pale, litakuwa la uumbaji, kwa sababu hilo ni Neno lililomea. Kwani, Mungu ni Neno, na Uzima wa Mungu uko katika Neno. Angalia sasa wakati lile Neno lilipodondoka ndani ya Uzima wa Mungu, kitu fulani kilitukia, hicho hutukia.

Sasa tazama. Ndipo Yeye alipomtokea Abrahamu katika Jina la Mungu Mwenyenzi. Sasa, Mungu anayo majina saba ya ukombozi yaliyounganika kufanya kuwa mmoja. Na Yeye alimtokea Abrahamu hapa katika umbo la Mungu Mwenyenzi ambalo humaanisha “El Shadai.” Katika... “Shadai,” katika Kiebrania. El humaanisha “mwenye nguvu.” Shad humaanisha “titi,” kama titi la mwanamke. Na sasa badala ya kuwa “shad,” umoja; “Shadai,” wingi. Sasa ni faraja tamu iliyoje kwa mwanamume mzee, mwenye umri wa miaka mia, akishikilia Neno la Mungu moyoni mwake, na kuisikia Sauti ya Mungu ikimjia na kusema, “Mimi ni El Shadai. Mimi ni Mungu mwenye Matiti.”
Tunayo faraja iliyoje! Sasa, sasa, kumbuka, siyo tu ‘mwenye matiti,’ bali ‘mwenye matiti’! Aliyejeruhiwa kwa ajili ya maovu yetu; kwa kupigwa Kwake sisi tulipona.”

Sasa, mama hufanya nini, kwa mtoto wake mdogo, mtoto awapo mgonjwa na kutaabika? Yeye humchukua yule jamaa mdogo. Yeye humshikilia kwenye titi lake, na mama... na yeye hunyonya nguvu za mama yake na kuingiza katika mwili wake mwenyewe kupitia titi. Na siyo tu yeye anatosheka au yeye... Yeye anatulizwa. Yeye anapiga kelele kwa sauti yake ya juu, yeye anakuwa amesumbuka sana; lakini yule mama anapomnyanyua na kuweka... kumweka kwenye titi, na kuanza kumvumishia wimbo, akimtingisha nyuma na mbele kumbembeleza mtoto, yeye anamhisi mama yake, kichwa chake kinakuwa juu ya kifua cha mama, na yeye anaanza kunyonya na kuvuta nguvu kutoka kwa mama yake, kuingiza ndani ya mwili wake. Yeye anajipa tena afya mwenyewe, akijenga nguvu; na pia kutosheka, wakati siku kwa siku yeye anakua na nguvu zaidi na zaidi.

----
El Shadai! Yeye alisema, “Mimi ni El Shadai. Abrahamu, Mimi ni Mwenye nguvu. Wewe ni mzee. Wewe una umri wa miaka mia. Sasa, nguvu zako zimekwisha; lakini Mimi ndiyo Nguvu zako! Tumaini lako lote limeondoka; lakini Mimi ni Tumaini lako! Ee, ukiteseka, jioni hii, na nje hapa ukiwa na saratani na vitu, je, huwezi kuona Nguvu zako zinatoka wapi? Siyo kutoka kwenye kisu cha daktari mpasuaji, bali kutoka kwenye Neno la Mungu! “Mimi ni Sehemu yako! Mimi ni Nguvu zako! Unavuta nguvu zako kutoka Kwangu!”

Siyo kumpuuza daktari mpasuaji sasa; yeye hufanya sehemu yake ambayo ni juu yake. Lakini Mungu ndiye Mponyaji. Hakuna daktari mpasuaji, hakuna daktari, hakuna dawa iliyowahi kuponya. Hapana, bwana, wao hawana dawa hata moja itakayoponya. Sasa, daktari yeyote atakuambia hilo! Wao wanayo misaada, lakini Mungu ndiye Mponyaji. Wao wanaweza kukata mshipa katika mkono wako, lakini inampasa Mungu auponyeshe huo. Wao hawana chochote cha kujenga misuli ya mwili; kama wangeweza, wao wangemtengeneza mtu. Hivyo mnaona, Mungu ndiye Mponyaji. Unaweza kurekebisha mfupa, lakini Mungu inampasa auponye huo. Mungu ndiye Mponyaji, “Mimi ni Bwana nikuponyaye magonjwa yako yote.” Na huwezi kufanya Neno la Mungu liseme uongo; litarejea moja kwa moja kwenye ukweli kila wakati, litarejea tu moja kwa moja. Huwezi kulifanya Hilo liseme uongo.

----
Sasa, Abrahamu alipopata hili neno, kuwa, “Mimi ni El Shadai. Mimi ni Mpaji-Nguvu wako! Mke wako, tumbo lake la uzazi limekwishakauka, yeye amekwishakupita hali yake ya kike kwa miaka arobaini, mwili wako ni kama uliokufa; lakini Mimi ni El Shadai.” Yeye alimleta tu Ishmaeli, un anajua; lakini Yeye alisema, “Siyo huyo. Hapana, yeye atakuwa mtu mkuu. Yeye anakwenda kuwazaa wafalme wengi mno. Lakini yule niliyefanya ahadi, ni kati yako na Sara.” Hilo ndilo jambo lenyewe! Amina. Abrahamu alijisikia vizuri hasa. Yeye alisema, “Sasa nataka nikuambie jambo fulani, Abrahamu. Mimi nakwenda kubadili jina lako.” Yeye alisema, “Wewe hutaitwa tena Abramu, bali Abrahamu.” Abramu humaanisha “baba wa juu-juu.” Lakini Abrahamu humaanisha “baba wa mataifa.” Na siyo S-a-r-a-i tena; yeye ni S-a-r-a, Sara, “malkia.” Alibadili jina lenu! Ni jina lililobadilishwa iliyoje! Jambo fulani lilitukia kwa sababu wana... Unaona, inapasa pawepo na badiliko kabla mambo hayajatukia. Yeye hakuweza kuwapa mtoto maadam majina yao yalibakia hivyo.

Nawe huwezi kuzaliwa mara ya pili maadam jina lako linabakia nje ya Kitabu cha Mbinguni. Unaweza kuliweka hilo kwenye kila kanisa, Methodisti, Baptisti, Presbiteri, ukilichukua kutoka mahali hadi mahali, ukihangaika na wote; lakini inapasa hilo liwekwe kwenye Kitabu cha Mbinguni kabla kitu chochote hakijaweza kutukia, na uumbaji mpya unaweza kuja. Kabla uzima mpya haujaja, majina yao inapasa yabadilishwe. Mwaweza kubadili yenu, pia, kutoka kwenye baadhi ya hivi vitabu vilivyotengenezwa na mwanadamu, kwenda kwenye Vitabu vya Mbinguni.
“Na pale, jina lako siyo tena Abramu, ‘baba wa juu’, bali ni Abrahamu, ‘baba wa mataifa.’ Siyo (Sara) Sarai tena, Sarai; bali Sara, ‘malkia’!”

----
Siku moja jua lilichomoza likiwa na joto hasa asubuhi moja, Abrahamu alikuwa ameketi kivulini mwa hema lake pale kando ya mwaloni. Na yeye akatazama chini, ni lazima ilikuwa penye saa tano asubuhi, na yeye aliwaona watu watatu wakija, wakija juu, nguo zao zikiwa na vumbi. Na Abrahamu akakimbilia nje. Kulikuweko na kitu fulani moyoni mwake kilichomfanya ajisikie vizuri hasa, na yeye akakimbilia nje na kuanguka miguuni pao. Na tazama, yeye alisema, “Bwana wangu!” Je, hilo si la ajabu? Watu watatu; lakini, “Bwana wangu”!

Mtazame Lutu. Wakati hao wawili walipokwenda chini kule, hao wawili tu, yeye alisema, “Mabwana zangu.” Lutu aliwaita wao “mabwana.” Abrahamu...Lutu aliwaita, wawili, “mabwana.” Na Abrahamu aliwaita hao watatu, “Bwana! Bwana wangu!” Amina! Ee, wakati umekaribia! Tazama, yeye alisema, “Bwana wangu, kama nikipata neema mbele Zako, uje, uketi chini ya mwaloni. Hebu mimi nilete maji kidogo na nioshe miguu Yako, na ule kiasi kidogo cha mkate. Kwani hii ndiyo sababu pekee ya Wewe kuja hapa, ili kuniona mimi.” Wao wakatembea kule.

Abrahamu alitoka nje na kwenda nyuma ya hema, na kusema, “Sara, kakande donge utengeneze kwa haraka, na utengeneze keki juu ya jiko.” Akatoka nje na kumkamata ndama mdogo, na kumchinja na kuandaliwa, na kutengeneza vipande vya nyama, na kuleta siagi na maziwa, na-na kuviweka chini mbele za yule Mtu, nao wakala. Na Mmoja wao alikuwa Mungu Mwenyewe! Hilo ndilo Biblia ililosema. Sasa kama unataka kubishana na Hilo, endelea. Abrahamu alimwita Yeye ‘Elohimu’, Mungu. Abrahamu alipaswa kujua; yeye alikuwa anazungumza na Yeye. Tazama, “Bwana Mungu!” Sasa, Mmoja wao alikuwa Mungu. Na Abrahamu alimtazama Yeye. Abrahamu akalitambua hilo. Sasa tazama pale.

----
Tazama. Sasa tunaona, huyu Mtu aliketi chini na kula. Na wawili kati yao walisimama na kwenda chini Sodoma. Mmoja alikaa na Abrahamu. Hebu tutazame mazungumzo yao. Waliendelea kutazama kuelekea Sodoma. Na Abrahamu alijua kulikuweko na kitu fulani cha kigeni kidogo juu ya huo. Hivyo Yeye akasema, basi Yeye alipokuwa tayari kuondoka, Yeye alisema, “Unafikiri nitamficha Abrahamu; yeye akiwa anakwenda kuwa baba wa mataifa, najua jinsi yeye atakavyowalea watoto wake, na kadhalika; hicho kitu ninachokwenda kufanya?” Yeye akasema, “Dhambi za Sodoma zimehuzunisha mno hadi imeingia masikioni Mwake.” Yeye ameshuka chini kuchunguza.

Sasa kumbukeni, kama nilivyosema usiku ule mwingine, wawili kati ya hao wajumbe walikwenda chini katika Sodoma, nao waliwahubiria hao Wasodoma; na waliwapofusha hao usiku ule, kwenye Neno. Lakini, kumbukeni, kulikuweko na Mmoja; wao, walikuwa na ishara yao, Mgeni miongoni mwao.
Mtazame Lutu. Lutu ameketi penye lango, na kusema, “Mabwana zangu.” Na kuishi namna hii! Wao walisema, “Ingieni nyumbani mwangu.” Yeye alisema, “Sisi tutalala barabarani.” Ni nyumba iliyoje!
Lakini mara tu Abrahamu; wao walisema, “Hili ndilo kusudi tulilojia. Tutaketi chini hapa kando yako.”

Hiyo ndiyo njia. Ishi hivyo, kwamba kama Mungu angelitaka kukutumia, Yeye anajua pale pale pa Yeye kuja ili kukupata. Wewe uko katika nafasi, ukiishi ukiwa maisha safi mbele za Mungu, maneno yako ni ya ukweli. Hapo ndipo aina ya mahali ambapo Malaika huja. Mtazame Elizabethi na Zakaria, unaona, msimamo mwadilifu, wakitembea katika Amri zote za Bwana. Hivyo ndivyo tunavyotaka kuishi, hivyo Mungu anapokuwa tayari kukutumia, Yeye anasema, “Hawa ni watu Wangu. Naweza kufanya kile ninachotaka na hili kanisa. Wao wananiamini Mimi. Wao wanasimama juu ya Neno Langu.” Unaona. Hivyo ndivyo unavyotaka kufanya, ishi hayo maisha.

Sasa tunakuta huyu Malaika, Yeye alisema, “Sitamficha Abrahamu. Lakini nitakutembelea kulingana na wakati wa furaha mno.” Na tazama, Yeye hakumwita Abram, Yeye alimwita “Abrahamu.” Mungu alijuaje kuwa hilo jina lilikuwa limebadilishwa? Yeye alikuwa Ndiye aliyebadili hilo. Hakika. Tazama, kamwe hakumwita Sarai, unajua, S-a-r-a-i, S-a-ra, “Mkeo yuko wapi, Sara?” Mungu alijuaje kuwa yeye alikuwa ameolewa? Yeye alijuaje Abrahamu alikuwa na mke, na jina lake lilikuwa Sara?
Na Abrahamu alisema, “Yeye yuko katika hema nyuma yako.”

----
Tazama, hilo lilikuwa pale. Sara alikuwa ndani ya hema, yeye alikaa ndani mle na kujiheshimu. Abrahamu alikuwa anafanya makaribisho ya hawa Malaika. Sasa, na Yeye alisema, “Nitakutembelea.”
Na Sara alikuwa anasikiliza. Na yeye alicheka kimoyomoyo, akasema, “Mimi, mwanamke mzee, nikiwa mzee kama nilivyo, na pale bwana wangu mzee pia, na aseme kuwa tunakwenda kuwa na furaha tena kama mume na mke?” Na yeye akacheka. Na yule Malaika, akiwa amepiga kisogo, alisema, “Mbona Sara amecheka?”
Kumbukeni, hiyo ilikuwa ishara ya mwisho ambayo ule Uzao wa... au Abrahamu mwenyewe, ambao ni mfano wa Kanisa, hiyo ilikuwa ishara ya mwisho ambayo yeye aliipokea. Katika ishara zote zile nyingine ambazo yeye alizipokea, hiyo ilikuwa ya mwisho kabla Sodoma haijaangamizwa. Je, hilo ni sahihi? Ile ishara ya mwisho!

----
Ilikuwa ni kitu gani? Mungu akiwaandaa Sara na Abrahamu ili kupokea mwana wa ahadi. Ikionyesha kuwa jambo linalofuata baada ya udhihirisho wa huyu Malaika wa Mungu, Roho Mtakatifu akionyesha ishara Yake ya mwisho, jambo linalofuata, huu wa kufa unachukua kutokufa na tunachukuliwa juu hewani ili kukutana na Mwana wa ahadi, Mzao wa kifalme wa Abrahamu. Utukufu kwa Mungu! Haleluya! “Kwani tutabadilika katika kitambo kifupi kufumba na kufumbua, nasi tutachukuliwa juu pamoja ili kukutana na Yeye hewani. Hivyo tutakuwa pamoja na Yeye, Mwana wa ahadi.” Haleluya!

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Yehova-Yire #2.