Mungu alikuwa amefichwa katika Yesu.

<< uliopita

ijayo >>

  Siri hiyo ya Kristo mfululizo.

Kufunuliwa kwa Mungu.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Kufunuliwa kwa Mungu.

Sasa somo langu asubuhi hii ni kudhihirisha, au kumfunua huyo Mungu. Mungu daima katika kila kipindi Amekuwa akijificha nyuma ya pazia vipindi vyote, lakini Amekuwa Mungu wakati wote. Mnaona? Lakini amedumu kujificha ulimwengu usimwone, na Anajiweka wazi Mwenyewe kwa Wateule Wake, kama mitume wa siku ile. Sasa, huyo ni Mungu aliyekuwa akisema katika Kristo.

Wakati mmoja Musa alitamani kumwona Mungu, na Mungu akamwambia asimame juu ya mwamba. Na, Musa alisimama juu ya ule mwamba, na akamwona Mungu akipita, na mgongo wake ulionekana kama mgongo wa mtu. Mungu alikuwa katika tufani, na Mungu... wakati Musa alipokuwa amesimama juu ya mwamba. Nadhani nyote mmekwishaona ile picha nje pale, siku ile, tulisimama kando ya ule mwamba. Na hii indiyo ile Nuru, Malaika wa Mungu pale pale ulipotokea mgongano. Alisimama... Hii ipo pale penye ubao wa matangazo sasa tena.

Tazama, Yehova wa Agano la Kale ndiye Yesu Kristo wa Agano Jipya. Unaona? Ndiye Mungu huyo huyo, huwa tu anabadili mionekano.

----
Mungu alijibadilisha, Alibadilisha umbo lake. Kama ukiangalia hapa katika Wafilipi, Alisema, “Hakuona ni kitu cha kushikamana nacho, bali alivaa umbo la mwanadamu”. Sasa, tafsiri ya Kiyunani ya neno umbo, nimekuwa nikitafuta mchana kutwa jana, nikijaribu kufikiri ilikuwa ni nini, nilikuta nimekuja na neno “en morphe”. Herufi zake zilikuwa e-n-m-o-r-p-h-e. Nilipotafuta katika Kiyunani nipate en morphe ilikuwa nini... Ningeweza kutamka kimakosa, lakini nika... ndiyo sababu nikataja herufi zake, ili kwamba kanda zitakapotolewa kwa watu, watu wata (wasomi wata) jua kile nina-ninachomaanisha kuhusu hilo. Yeye... Wakati en morphe... Hiyo inamaanisha kwamba Yeye alijibadilisha Mwenyewe. Yeye- Yeye alishuka chini. Sasa, neno la Kiyunani pale lilimaanisha kuwa kitu kisichoweza kuonekana, ila kipo na ndipo kikawa kimebadilika na jicho likaweza kukiona.

----
Na huyo ni Mungu. Alijibadilisha Mwenyewe kutoka-kutoka Nguzo ya Moto, kuwa Mwanadamu. Ndipo Akajibadilisha Mwenyewe kutoka hilo kurejea kuwa Roho tena, ili aweze kukaa ndani ya mtu. Mungu akitenda kile alichokuwa hali akiwa ndani ya mtu. Yesu Kristo alikuwa Mungu akitenda akiwa ndani ya mtu, ndani ya mtu, ndani ya mtu. Hicho ndicho Alichokuwa. Alijibadilisha kutoka Nguzo ya Moto, na ndipo alikuwa amekuja ndani yake, ambayo ilikuwa ni pazia tu kule jangwani lililomficha Mungu Israeli wasimuone. Musa aliona umbo la mwili Wake, ila kwa kweli Alikuwa amefichwa wakati wote nyuma ya hii Nguzo ya Moto, ambayo ilikuwa ndiyo Neno yule Aliyetoka kwa Mungu.

Sasa tunakuta hapa, sasa, tangu Pentekoste, Mungu hatendi akiwa katika umbo la mtu au kutenda... sasa anatenda akiwatumia watu. Unaona? Alikuwa akitenda akiwa ndani ya mtu wakati huo, Yesu. Sasa anatenda akiwatumia watu aliowachagua kwa kusudi Lake. Mungu katika umbo la mtu. Yeye Alijibadilisha Mwenyewe kutoka umbo la-la-la Mungu kuwa umbo la mtu.

----
Tazama sasa wakati Alipokuja, ilibidi aje akiwa Mwana wa Adamu kwa sababu ndivyo Maandiko yalivyosema Angekuja. Mungu angewainulia aje kwao. Hivyo Asingekuja na kujiita Mwana wa Mungu, kwani hakikuwa kipindi cha Yeye kuwa hivyo. Alikuwa Mwana wa Adamu akitoa unabii, ili kutimiza, na kudhihirisha kwao wote, mambo yote yaliyokwishatendeka na kuwa kivuli cha kile Yeye alichokuwa. Basi Alikuwa duniani kama Mwana wa Adamu.

----
Mungu amejimimina Mwenyewe kumjaa mtu, Yoeli 2:28, tunakuta, Alisema, “Nitamwaga Roho yangu katika siku za mwisho”. Na kama utaangalia neno lililoko pale, neno la Kiyunani... Ninaweza nikawa nimekosea, lakini lile nililolipata...

Inakupasa ulichunguze hili neno. Kiingereza mara nyingine huwa na maana mbili za neno moja. Kama tu, neno tunasema, “mungu”. Mungu aliumba mbingu na nchi Mwanzo 1. lakini sana, katika Biblia ilisema, “Hapo mwanzo Elohim, ”Sasa, Elohim. Katika Kiingereza iliitwa, “mungu”, lakini kwa kweli haikuwa Elohim. Kitu chochote kile chaweza kuwa mungu kwa neno hilo mungu: Unaweza kukifanya kuwa mungu, unaweza kukifanya kile kinanda kiwe mungu, unaweza kukifanya kila kitu kiwe mungu. Lakini sivyo ilivyo katika neno Elohim, Inamaanisha “Yeye pekee Aliyeko”. Unaona? Kile kinanda hakiwezi kuwa kilicho pekee kilichopo, hakuna chochote kinachoweza kuwa kile pekee kilichopo. Kwa hiyo lile Neno Elohim linamaanisha “Yule ambaye Amekuweko tangu kale na kale”. Mungu inaweza kumaanisha kitu chochote. Unaona tofauti katika hilo neno?

Sasa, wakati liliposema hapa kuwa Alijimimina Mwenyewe, au Alijimwaga, sasa, tunafikiri hivi, kuwa, Yeye “alitapika”, neno la Kiingereza la kujimimina au kujimwaga kutoka ndani Yake Mwenyewe, unaona, kitu fulani kutoka ndani Yake kilichokuwa tofauti na Yeye Mwenyewe. Lakini neno Kenos, katika Kiyunani halimaanishi kuwa Yeye “Alitaapika au kitu... mkono Wake ulitoka au jicho Lake lilitoka nje, nafsi nyingine.

Na hiyo ni, Alijibadilisha Mwenyewe, “Yeye Alijimwaga ndani ya” (Amina!) ndani ya kinyago, ndani ya umbo jingine. Siyo nafsi nyingine iliyotoka kutoka ndani Yake, iitwayo Roho Mtakatifu, lakini ilikuwa ni Yeye Mwenyewe. Unalipata hilo? Yeye Mwenyewe Alijimimina Mwenyewe ndani ya watu. Kristo ndani yako! Ni zuri jinsi gani, ni la ajabu jinsi gani, kuwaza juu ya, Mungu kujimimina Mwenyewe ndani mwanadamu, ndani ya mwamini. Alijimwaga! Ilikuwa sehemu ya tendo lake la igizo, kufanya hivyo. Mungu, ukamilifu wote, Uungu wote kwa jinsi ya mwili ulikuwa ndani ya huyu Mtu, Yesu Kristo. Yeye Alikuwa Mungu, na Mungu pekee. Siyo nafsi ya tatu,au nafsi ya pili au nafsi ya kwanza, lakini ile Nafsi yenyewe, Mungu aliyefichwa na mwili wa kibinadamu.

1Timotheo 3:16, “Na bila shaka siri ya utaua ni kuu; kwani M-u-n-g-u, Elohim...” M-u-n-g-u kwa herufi kubwa, katika Biblia, ukirejea huko nyuma, yeyote ambaye inamtaja katika maandiko yale ya kwanza, Ilimsema, “Elohim, Hapo Mwanzo, Elohim”. Mnaona? Na Elohim... Bila shaka siri ya Elohim ni kuu, kwani Elohim Alifanyika mwili, na tukamtazama“. Elohim akiwa amefunikwa na mwili wa kibinadamu! Yule Yehova mkuu aliyejaza anga lote, muda na kila mahali, alifanyika kuwa mwanadamu. Tulimpapasa Yeye, Elohim. Hapo mwanzo Elohim. Na Elohim akafanyika mwili, akakaa kwetu”.

----
Ni nani huyu Mtu mkuu asiyeonekana? Ni nani Huyu ambaye Abraham alimwona katika maono? Mwishoni kabisa hata ijapo Yeye alijidhihirisha katika mwili, kabla yule mwana hajaja, Mungu Mwenyewe alikuja kwa Abraham katika umbo la mwanadamu, wakati wa mwisho. Aliyedhihirishwa! Alimwona Yeye katika Nuru kidogo wakati fulani, alimwona Yeye katika maono, alisikia Sauti Yake, mafunuo mengi, lakini muda mfupi kabla ya kuja yule mwana wa ahadi, alimuona katika umbo la mwanadamu, na akazungumza Naye, na akamlisha nyama na kinywaji. Unajua? Tazama, Mungu Mwenyewe aliyefunikwa na pazia la mwili wa kibinadamu.

Hii ilikuwa sehemu ya njia Yake. Hii ndiyo njia ambayo kwayo anajidhihirisha Mwenyewe kwetu, anadhihirisha Neno la Milele, Mungu, Yehova aliyefanyika mwili. Kama katika Yohana 1, “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, Naye Neno Alikuwako kwa Mungu, na... Hapo Mwanzo kulikuwako Elohim, Naye Elohim akafanyika kuwa Neno. Naye Neno Alifanyika kuwa Elohim”. Unaona? Ni jambo lile lile likiendelea kuwa wazi tu.

Kama tabia ya asili, unaona, iko ndani ya Mungu. Tabia yako ya asili ni wazo lako. Mungu hapo mwanzo, Yeye Aliye wa Milele, Hakuwa wala Mungu, Mungu ni kile kinachoabudiwa, au kitu fulani. Mnaona? Hivyo wala hakuwa hicho. Yeye Alikuwa Elohim, Yule wa Milele. Lakini ndani Yake mlikuwemo Mawazo. Yeye alitaka kufanyika kuwa kitu halisi. Na Yeye alifanyika nini? Ndipo Yeye Alisema Neno, Naye Neno akafanyika kitu halisi. Hiyo ndiyo picha nzima kutoka kitabu cha Mwanzo hadi Ufunuo. Hakuna kosa lolote. Ni Elohim Akifanyika kitu halisi ili Aweze kuguswa, Aweze kupapaswa. Na katika Utawala wa Kristo wa miaka elfu moja kuna Elohim ameketi katika Kiti cha Enzi, unaona, hiyo ni sahihi, Akiwa pamoja na wote walio Wake, wale Aliowachagua tangu asili kabla ya kuwekwa msingi wa ulimwengu.

----
Tazama, katika vipindi mbalimbali, namna hiyo hiyo, Amejidhihirisha Mwenyewe. Wao hawakuwa manabii pekee tu, walikuwa Mungu. Yeye Alisema hivyo. Kwani kile walichokisema kilikuwa Neno la Mungu. Wao walikuwa miili iliyomficha Mungu. Walikuwa miungu. Yesu Mwenyewe, Alisema, “Mnawezaje kunihukumu Mimi ninaposema kuwa Mimi ni Mwana wa Mungu, na sheria yenu wenyewe inasema kuwa wale ambao Neno la Bwana lilikuja kwao walikuwa miungu? Mnaona?

Hivyo ilikuwa ni Mungu aliyeumbika katika mtu aliyeitwa nabii. Unaona? Na Neno la Bwana lilikuja kwa mtu huyu, hivyo haikuwa yule nabii, yule nabii alikuwa pazia, lakini Neno lilikuwa Mungu. Neno la mwanadamu haliwezi kufanya hivyo. Unaona ninachomaanisha? Haliwezi kukaa katika hali hiyo. Lakini kimsingi ilikuwa ni Mungu. Unaona, Yeye alikuwa ni Neno la Mungu katika umbo la mwanadamu, akiitwa “mwanadamu”. Tazama, Yeye hakubadili kamwe asili Yake, ila tu umbo Lake. Waebrania 13:8 ilisema, “Yeye ni Yeye Yule jana, leo na hata milele”. Kwa hiyo Yeye hakubadili asili Yake wakati alipokuja. Yeye amekuwa daima yule Nabii, moja kwa moja kupitia katika kipindi chote, kitu kile kile, Lile Neno, Lile Neno, Lile Neno. Unaona? Yeye hawezi kubadili asili Yake, lakini alibadili umbo Lake, Waebrania 13:8 ilisema “Yeye ni Yeye Yule jana, leo, na hata milele”. Yeye alibadili tu kinyago Chake.

----
Mungu alikuwa amefichwa katika Yesu, ili kufanya kazi ya ukombozi pale msalabani. Mungu akiwa Roho asingeweza kufa, Yeye ni wa Milele na Milele. Lakini ilibidi avae kinyago ili aweze kufa. Yeye alikufa, lakini isingewezekana kufa akiwa katika umbo Lake la Mungu. Ilibidi afanye hivyo akiwa katika umbo la Mwana, kama Mwana wa Adamu, hapa duniani. Mnaona? Ilipasa tu awe katika umbo la Mwana. Ndipo Yeye aliporudi siku ya Pentekoste, alikuwa Mwana wa Mungu tena. Mnaona ninachomaanisha? Umepata hilo wazo? Yeye ali...

----
Yeye amefunikwa na pazia ndani ya mtu, kama ambavyo siku zote amekuwa amefunikwa. Lakini kwao Yeye alikuwa amefunikwa na pazia, Yeye alikuwa katika hekalu Lake. Mungu alikuwa katika hekalu la kibinadamu. Tafadhali uwe makini kweli kweli, sasa Yeye ni Yeye Yule jana, leo, na hata milele. Mnaona, Mungu akiwa amefunikwa na pazia, akiwa amejificha ulimwengu usimwone, Yuko ndani ya pazia la mwanadamu. Unaona?

Yeye alikuwa Mungu! Hao Wayunani wakisema, “Tunataka kumwona Yeye”, na Yesu akasema, “Chembe ya ngano sharti ianguke na kufa”! Ni sharti ufe katika fikra zako. Yabidi utoke katika mawazo yako mwenyewe. Kama ilivyokuwa kwa wale wanafunzi, hawakuweza kueleza kuhusu kuula mwili Wake na-na kuinywa damu Yake, lakini, ona, walikuwa wamekufa kwa hayo mambo. Walikuwa wamekufa wawe katika Kanuni, walikuwa wamekufa wawe kwa Kristo. Hata kama Yeye alifanya kitu gani, au Alivyoonekana kushindwa hata hivyo bado waliendelea kuamini Hilo. Unaona? Waliweza kuona ndani ya huyo Mtu... Mtu aliyekula, aliyekunywa, aliyevua samaki, aliyelala, aliyefanya kila kitu kingine, alizaliwa hapa duniani, na akatembea pamoja nao, akazungumza nao, akavaa nguo kama wengine wote, lakini huyo alikuwa Mungu.

----
KatikaAgano la Kale Mungu alifichwa wakati alipokuwa penye kiti Chake cha rehema, kwa kufichwa na pazia! Katika Agano la Kale, Mungu alikuwa katika hekalu Lake. Lakini watu waliingia na kuabudu namna hii, lakini, kumbuka palikuwepo na pazia (amina) lililomficha Mungu. Walijua kwamba Mungu alikuwa pale. Hawakuweza kumwona Yeye. Ile Nguzo ya Moto haikuonekana tena kamwe pale. Je, mling,amua hilo? Hakuna wakati wowote katika Maandiko, tangu wakati Nguzo ya moto ilipoingia na kukaa nyuma ya pazia, kwamba Yeye aliwahi kuonekana tena, hadi Ilipokuja kuonekana kutoka Kwake Yesu Kristo? Mungu Alijificha nyuma ya pazia!

Wakati Yeye aliposimama duniani Alisema, “Mimi ninatoka kwa Mungu na Ninakwenda kwa Mungu”. Ndipo Paulo, (baada ya Bwana kufa, kuzikwa na kufufuka), akiwa njiani kwenda Dameski, Ilikuja tena ile Nguzo ya Moto. Ilikuwa nini? Ilitokea nyuma ya lile pazia! Utukufu kwa Mungu!

Yeye alikuwa katika nyuma ya pazia. Sasa, alikuwa nyuma ya nini? Pazia la ngozi. Unaona, “ngozi ya pomboo”, nyuma ya pazia. Na lile pazia lilipopasuka siku ile ya kusulubiwa, lile pazia ambalo Yeye alikuwa amefunikwa nalo lilipasuka siku ile ya kusulubiwa, kiti chote cha rehema kikaonekana wazi. Sasa Wayahudi hawakuweza kuelewa ni kwa jinsi gani kwamba Mungu angeweza kuwa na rehema juu ya watu wenye dhambi, wakosaji kama sisi tulivyo. Lakini hawakuweza kumwona huyu Mmoja Ambaye alikuwa anatoa rehema, kwa sababu alikuwa amefichwa. Yeye alikuwa nyuma ya kiti cha rehema, mle ndani, akiwa na ngozi ya pomboo zikining,inia chini kumfunika Yeye.

Kabla, kama ali... Kabla, kama mtu yeyote alipita nyuma ya pazia, ilikuwa ni kifo mara moja. (Oh tunakwenda kupata somo hapa kitambo kidogo, unaona, kama una... kama utaweza kulikubali.) Kujaribu kupita nyuma ya zile ngozi, hata mmoja wa wana wa kuhani alijaribu kufanya hivyo wakati mmoja na akafa. Usiende nyuma ya lile pazia. Yule mtu aliyepita nyuma ... Kwa nini? Hapakuweko na ukombozi mle wakati huo. Ilikuwa kimsingi, ilikuwa tu kimsingi; na chochote kilicho kimsingi, sicho kile kitu chenyewe halisi bado, unaona, ni kimsingi tu. Ilikuwa ni ukombozi... Dhambi ilifunikwa, haikurukwa... namaanisha, haikuondolewa, haikufutwa. Kufutwa inamaanisha “kuondolewa na kutupiliwa mbali”. Na hivyo damu ya kondoo na mbuzi haingeweza kufanya hilo, hivyo Yehova alifichwa nyuma ya pazia. Sasa, huko nyuma ya pazia hili pale ambapo Yeye alifichwa, kuingia ndani mle, mtu alianguka na kufa, kwa kule kujaribu kuingia mle ndani.

Lakini tangu Pentekoste, tangu Usulubisho, wakati lile pazia lilipopasuka toka juu hadi chini, kwa ajili ya kile kizazi... Yesu Alikuwa Yule Mungu aliyekuwa amefichwa na pazia. Na Yeye alipokufa pale Kalvari, Mungu alituma moto na umeme na kupasua lile pazia kutoka juu hadi chini, hata kiti chote cha rehema kilikuwa peupe. Lakini walikuwa vipofu kupita kiasi hata wasilione Hilo. Kama Musa alivyosema hapa, Paulo alisema akisoma juu ya Musa, “Wakati Musa akisomwa, bado ule utaji bado unakuwepo juu ya mioyo yao.” Ee ndugu, dada, hicho ndicho Wayahudi walichofanya wakati lile pazia liliporaruka na kumweka Mungu penye uwazi, akiwa ametundikwa msalabani. Yeye alikuwa katika uwazi, lakini wao hawakuweza kuliona Hilo.

----
Mungu ambaye hakufunikwa na pazia, aliye katika uwazi, wangekuwa wamekwishamwona Yeye akiwa amesimama pale. Bado alikuwa amefahamika na kila mtu wa kawaida kiasi, Yeye alikuwa mtu wa kawaida. Wao hawakuweza kuliona Hilo. Mnaona, pale alisimama mtu, “Vyema,” walisema, “huyu jamaa, alisomea shule gani?” Lakini kumbuka, wakati ule mkuki ulipochoma mwili wake, yule Roho alimwacha Yeye, lile hekalu... lile sanduku la dhabihu lilipinduliwa, na umeme ulimulika chini kupitia hekaluni na kurarua lile pazia. Ilikuwa kitu gani? Pale ilikuwa ni Mungu wao amening,inia pale Kalvari, na walikuwa vipofu kupita kiasi hata wasione hilo. Walimleta katika uwazi, na bado wasilione Hilo! Wao ni vipofu. Mungu aliyefichwa na pazia la mwanadamu!

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Kufunuliwa kwa Mungu.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Forerunner.

Jina la Mungu.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni apple?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

  Maandiko Anasema...

Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.

1 Timotheo 3:16


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDF Kiingereza)
 

Chapter 11
- The Cloud

(PDF Kiingereza)
 

William Branham Life
Story.

(PDF Kiingereza)

How the Angel came
to me.
(PDF Kiingereza)



Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.