Kutoka kwa Tatu.


  Mfululizo wa wakati wa mwisho.

Kutoka Kiroho.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Kutoka kwa Tatu.

Sasa, wamekuwa na kutoka kwingi, lakini nazungumza juu ya ule wakati ambao Mungu aliuita kutoka, kutengana na pale walipokuwa kwa wakati huu. Mungu hapa anakuwa tayari kutimiza Neno Lake la Ahadi ya Kiungu alilowapa Abrahamu, lsaka, na Yakobo. Miaka, miaka mamia ilikuwa imekwishapita, lakini bado, Mungu kamwe hasahau ahadi Yake. kwa majira, wakati uliokubalika, Mungu siku zote hutimiza ahadi Yake. Kwa hiyo, unaweza kuwa na hakika kuwa kile Mungu. alichoahidi katika Biblia hii, Yeye atakifanya. Hakuna tu haja ya kujaribu kuwaza chochote kile na kusema, “Vema, nabii alikuwa-labda alikosea, au hilo Iisingeweza kutokea katika hii siku.”

Ilionekana kama lisilowezekana wakati ule, lisilowezekana kuliko inavyoonekana sasa, lakini Mungu alilifanya hata hivyo, kwa sababu Yeye aliahidi angelifanya hilo. Na tazama jinsi Yeye anavyolifanya kirahisi: “Nimeshuka; nilisikia kilio; nalikumbuka ahadi Yangu, nami nimeshuka chini kulifanya hilo, nami nakutuma. Ulifanye hilo, nitakuwa pamoja nawe; hakika nitakuwa pamoja nawe. Uwepo Wangu kamwe, kamwe haushindwi utakuwa pamoja nawe popote utakapokwenda. Usiogope. Nashuka chini ili kukomboa.” Nina hakika akili ya kiroho inalidaka hilo. “Nitakutuma kuleta watu wangu watoke, uwaite watoke nje nami nitakuwa pamoja nawe.”

Sasa, jinsi gani-jinsi gani tunaweza kupumzika, jinsi gani imani inaweza kushika hilo tumaini pale. Mungu anakwenda kulifanya hilo; Yeye aliliahidi hilo. Haidhuru, hali zikoje, au asemacho yeyote yule, Mungu atalifimya hata hivyo, kwa sababu, Yeye aliahidi kufanya hilo. Na Yeye hulifanya kirahisi kiasi kwamba linapita juu ya ufahamu wa akili zilizoelimika, ambazo zingejaribu kufikiri kuhusu hilo. “Lawezekanaje?” Simaanishi kusema kuwa mtu sasa, mwenye akili imara, elimu nzuri, kwamba yule mtu hawezi kuielewa. Hiyo ni sahihi, vizuri sana ili mradi anatumia hiyo, sio kutoa hoja, ila ule utamaduni alio nao kwa kumwamini Mungu.

Hebu libadilishwe katika urahisi wa kusikiliza kile Mungu alichosema na ukiamini. Basi utamaduni Wake utamsaidia. Tazama, mtu anapojaribu kutoa hoja kuwa haliwezi kutendeka, basi hilo humpeleka mbali na Mungu, daima wakati wote. Wakati anapojaribu kusikiliza... ufahamu wake mwenyewe, unaona. Kama huelewi na Biblia inasema jambo fulani, liitikie tu, “Amina,” liache tu liende namna hiyo.

----
Kabla ya kujua huku kutoka kuma maana gani, nakwenda kufananisha kutoka wakati ule na kutoka sasa. Na angalia, kama haiendi sambamba hasa. Moja ni ya asili na jambo lile lile ambalo Yeye alilifanya katika asili. Anaufananisha tena, (kuleta uhalisi wake) katika kiroho. “Kutoka Kiroho.”

Inashangaza kuona Neno la Mungu-jinsi gani mtu yeyote angeweza kusema halikuvuviwa. Hii ni kwenye miaka 2800 iliyopita, unajua. Ni jinsi alivyoahidi na kile- Yeye alichofanya, na kukiweka pale kama mfano. Jinsi Yeye afanyavyo kivuli cha jambo fulani kushuhudia kile kilicho halisi.

Lakini kwanza, lazima tupitie upya Mwanzo tuone kwa nini walikuwa kule Misri? Kwa nini watu wa Mungu wangelikuwa nje ya ile nchi? Na hata hivyo Mungu aliahidi hilo pale pale mwanzo alipokuwa na Abrahamu, Isaka na Yakobo, katika Palestina. Mungu aliwapa ile nchi, na kusema, “Ndiyo hii.”

Vema, basi kwa nini wale watu wasiwe mahali pale alikowapa Mungu? Hilo ndilo swali la leo, pia. Mungu alitupa Pentekoste. Yeye alitupa Kitabu cha Matendo. Yeye alitupa Roho Mtakatifu Atuonyeshe njia na kutuongoza. Yeye alitupa nchi, na kwa nini tuko nje ya hiyo nchi? Kwa nini lile kanisa kuu la Kikristo leo haliishi tena kama Kitabu cha Matendo, likileta jambo lile lile? Kuna sababu yake.

Sote tunajua kuwa tumefilisika na tuko katika hali ya kutisha; na hali ya kutisha kuliko zote ambazo Ukristo umewahi kuishi ndani yake ni leo. Na tuko kwenye-moja kwa moja kwenye ukingo au karibu kabisa na hukumu kuu ya kutisha kwa ajlli ya kanisa, na kabla ya hii hukumu kutokea, Mungu anaita kutoka kama tu Yeye alivyofanya wakati ule.

Dhambi za Waamori zilikuwa zimelundikana. Kwa hiyo Yeye anaita kutoka kiroho. Sasa, hebu turudi nyuma kwa muda mfupi na tufananishe na tujue. Wao walikwenda Misri kwa sababu tu ya kumwonea ndugu. Hiyo ndiyo sababu ambayo Israeli walikuwa katika Misri kwa wakati ule, nje ya ile nchi. Kumbukeni, ahadi za Mungu zilikuwa tu pale ambapo walikaa katika ile nchi.

Sasa, unaweza kuona kile tulichokuwa tukisema katika maombi kitambo kidogo kilichopita? Kwa nini ilimpasa Mungu aufanye moyo wa farao kuwa mgumu? Kuwarudisha wale watu katika nchi.ya ahadi kabla Yeye hajawabariki, ili kuwaletea Masihi. Jinsi gani aliufanya moyo wa Hitler kuwa mgumu awe dhidi ya Wayahudi, wakati yeye mwenyewe alikuwa nusu Myahudi? Jinsi gani alifanya hilo katika Stalin, Mussolini?

Unaona, watu ambao hawajavuviwa, kama taifa, wao... Mungu inabidi achukue vitu ambavyo wanaishi navyo, mara nyingine ile sheria za nchi, ili afanye ahadi Zake zitokee kweli. Kwa Hiyo, Yeye ilibidi afanye mioyo ya wale watawala wa mabavu iwe migumu ili kuwarudisha Wayahudi kwenye nchi ya ahadi. Ilipasa iwe hivyo.

Sasa, tunakuta kuwa tukirudi nyuma, Yusufu... Tunaijua habari unaporudi katika kitabu cha Mwanzo, na unaweza tu kuIisoma kwa sababu, nimechelewa tu kidogo kuanza juu ya hili somo refu la shule ya Jumapili. Nitajaribu kuharakisha. Tazama, sasa, soma ile habari ya Yusufu ukiweza, akiwa amezaliwa mwishoni mwa ndugu zake, wa pili kutoka mwisho. Akili ya kiroho italidaka hilo sasa hivi. Yeye hakuwa mtoto wa mwisho; lakini katika kutengwa, tazama. Yusufu na Benyamini walikuwa ndugu wa damu kabisa, na ni hao wawili pekee waliokuwa ndugu. Benyamini hakuwahi kutambulika hadi alipokutana na Yusufu. Na zaidi ya hao wengine wote, Benyamini alipewa maradufu kwa kila kitu Yusufu alichotoa. Vema, tazama sasa, tunakuta kwamba chini kule, kulikuwa na...

Yeye aliondolewa toka kwa kaka zake kwa sababu yeye alikuwa wa kiroho. Yeye alikuwa mtu mkuu, ingawa yeye alikuwa mnyenyekevu kuliko wote katika kundi lile, mdogo kuliko wote katika lile kundi, na walimchukia bila sababu. Wasingepaswa wamchukie. Wangepaswa wamheshimu, kwa sababu... kwa nini walimchukia? Kwa sababu alikuwa ndugu? Sio hilo hasa. Walimchukia kwa sababu Mungu alijihusisha naye zaidi kuliko Yeye alivyokuwa kwa wale wengine wote. Mungu alimpa ufahamu wa kiroho. Yeye aliweza kufasiri ndoto kwa usahihi, naye aliweza kutabiri mambo kabla ambayo yalitukia kwa usahihi, kama tu hasa yalivyokuwahakujitapa hata kidogo.

Yeye aliota ndoto ya yale masuke yakipiga magoti mbele ya suke lake, nao ndugu zake wakamkasirikia. Wakasema, nadhani basi... “Wewe mtakatifu mdogo anayejiviringisha.” Kwa maneno mengine, “Tutakupigia magoti siku moja.” Lakini hivyo ndivyo ilivyotokea. Jinsi gani yale majitu makubwa yangepiga magoti mbele ya mtu mdogo mnyonge aIiyesimama pale, lakini walifanya hivyo. Hakika walifanya hivyo, na kuomba rehema. Lakini bado hakuwa katika mamlaka, unaona. Wakati ule alikuwa tu katika hali ya kitoto.

Na ndipo tunakuta kwa kufanya hili, Yusufu alichukuliwa toka miongoni mwa ndugu zake, madhehebu na akakaa mahali yeye mwenyewe-kaka zake wote katika nchi. Ndipo kunakuja jambo kuu. Tunatambua kuwa Israeli, ili mradi walikaa katika makao yao na kudumu-sasa hilo ni jambo moja zuri kukaa mahali ulipowekwa, hiyo ni sahihi, lakini walimwacha Roho.

Walio walokole leo, kwa usahihi wanajua kile walicho kwa kuelewa Biblia kiakili, lakini hakuna Roho. Wamemkataa Yusufu, wakamtoa nje. Hawakutaka chochote kuhusu huyo, kundi la watakatifu wanaojiviringisha; ni... Hatutaki chochote kuhusu Roho. Wamemtenga na ushirika, wakamwuza kwa ulimwengu. Walikuwa nje ya ushirika wao.

Sasa, kwa kufanya hilo, waliondolewa mahali pao, wakapelekwa Misri baadaye. Sasa, habari ya hawa ndugu wenye wivu ni mlingano mkuu bila shaka na upande wake wa kiroho leo. Sote tunatambua hilo, kwamba ni wivu mtupu, wivu mchafu, unaona. Hakuna usafi katika wivu, unaona si chochote ila wivu mchafu.

Wanapoona Biblia ile ile na asili ya Mungu yule yule aliyeandika Biblia, akijithibitisha Mwenyewe na ndipo wanalikataa hilo bila sababu, safi... vema, safi kama nilivyosema, ni wivu wenye takataka. Wakitazama Mungu akiponya wagonjwa, akifufua wafu. Mungu yule yule aliyeishi katika siku za mitume. lnjili ile ile waliyoiandika kwa ajili ya hii safari ya kiroho. Ni Mungu yule yule anayefanya mambo yale yale, hadi hakuna chochote ila wivu; ametenga na ushirika, na “hatutakuwa nalo hili miongoni mwa watu wetu,” unaona, wanawafukuza.

Walifikiri-wale ndugu, kwamba kamwe wasingekuwa na haja na mtu kama yule, kwa hiyo, “Kwa nini asiondolewe.” Hilo ndilo... jambo lile lile limetokea leo. Wanafikiri kuwa kwa sababu makanisa yetu yamekuwa ya kiakili, kwamba tuna makundi yaliyovaa vizuri zaidi, mashirika makubwa kuliko yote, zaidi... wachungaji werevu kupita wote, kwamba hatuna haja na Roho Mtakatifu kama ambavyo ilikuwa kule nyuma.

Kwamba wametosheka, kwa maneno mengine matendo hupiga kelele kuliko maneno, kwamba seminari zao na-bongo zao za asili na kujikusanya kwao pamoja na kujadili hili jambo, wanaweza zaidi kwa akili zao wenyewe kuweka kanisa katika utaratibu ulio bora kuliko ambavyo Roho Mtakatifu angeweza kufanya; kwa hiyo hawamhitaji tena. Ni kitu ambacho hatukihitaji leo.

Ni kwamba... siku za hilo zimekwishapita, Sasa, hilo siyo sahihi? “Hatumhitaji Roho Mtakatifu kuponya wagonjwa, tunao madaktari. Hatuhitaji Roho Mtakatifu kunena kwa lugha, sisi sote tu watu wenye akili nyingi.” Na unapofanya hivyo, unaondoa kamba ya tegemeo la uzima toka kwenye muundo wa maisha yako. Yesu katika siku Yake aliwaambia Wayahudi, “Hamkusoma kwamba lile Jiwe lililokataliwa limekuwa Jiwe Kuu la Pembeni, lile ambalo jengo lote linakaa juu yake?”

Sasa, mnaona ninalomaanisha? Nina hakika mnaweza kulipata hilo. Kwambasababu yake sasa, ni kwa sababu walifikiri kwamba kamwe wasingemhitaji, “Hatuwahitaji wanenaji kwa lugha. Hatuwahitaji wafasiri wa lugha. Hatuhitaji tena manabii wa Agano la Kale kutuweka katika utaratibu kwa Roho Mtakatifu. Tunalielewa hilo.”

Unaona, wamechagua mfumo uliofanywa na mwandamu kuchukua mahali pa Roho Mtakatifu. Kwa hiyo, kuna watu waliochaguliwa, wanayo majina yao kwenye Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo; hawawezi kulipokea hilo. Wana akili za kiroho-kwa hiyo, hawawezi kulipokea hilo. Hawawezi kulivumilia. Haidhuru kama baba na mama zao wameishi katika shirika gani la dini au kanisa.

Wakati kanisa linapotengeneza au kufanya... labda lisingesema hilo kwa usahihi. Loo, hapana, wasingetamka hilo kwa usahihi lakini matendo yao yanalithibitisha. Hapa kuna Neno, na Roho Mtakatifu analithibitisha miongoni mwa wale wakati Yeye anapowakusanya pamoja, kwamba Yeye bado anaponya wagonjwa, anafufua wafu, ananena kwa lugha, na kutoa pepo. Kwa hiyo, inategemea kile kilichoko ndani ya mtu.

----
Kanisa linajisikia kuwa halihitaji Roho Mtakatifu. Makanisa yatakuambia hivyo. Na mtu anaweza kusimama na kukupa maongezi ya kiakili na nusura akufanye uamini hilo. Sasa, hebu tusimame hapo kwa dakika moja. Je, Yesu hakusema kuwa hawa wawili watafanana sana na ingewadanganya wateule halisi kama ingeliwezekana? Mazungumzo ya kiakili yatakuwa yanavutia sana kwamba yangewadanganya watu... Ni injili, ni mtu ambaye anaweza kushika lile Neno kwa namna ambayo angeweza kumfanya mtu yeyote mwenye akili nyingi, ikiwa tu unaamini katika akili nyingi, wanamlaani Roho Mtakatifu na kuchukua njia ya binadamu. Tunaona hilo.

Sasa, hilo ndilo jambo lile lile walilowaza kuhusu Yusufu, nao wakamwondoa. Na kote katika Misri... ee jinsi gani tunaweza kuwaza... jinsi gani ningetumia masaa... Ungeweza kukaa hapa kwa miaka mitatu na kamwe usingeacha hilo soma, mchana na usiku, na bado uendelee kupata viini vikuu vya Roho Mtakatifu.

Akili za kiroho zinaweza kutazama kule Misri na kuona kuwa mateso yanakuja, zinaweza kuona Yusufu akichukuliwa ili kwamba mateso yaje. Na ndipo uone Mungu na gurudumu lake ndani ya gurudumu-kila kitu kikienda kikamilifu tu. Mtazame Potifa akimkataa Yusufu. Tazama ule uongo ukisemwa na uone Yusufu magereza na ndevu zake zilizorefuka, akiwa ametengwa na ndugu zake, lakini ghafla, Mungu akaingilia kati!

Jinsi gani tunaweza kuona liIe gurudumu ndani ya gurudumu likitembea-mpango mkuu wa Mungu ukiendelea kila kitu hadi kufikia huku kutoka, hadi wakati huu Yeye anapoita watu Wake warudi katika nchi tena, warejee katika mahali pao, katika nafasi zao, mahali ambapo ataweza kuwabariki na kumweka miongoni mwao Mmoja ambaye Yeye aliahidi Angelimweka miongoni mwao. Iliwapasa wawe katika nchi yao. Kumbukeni, iliwabidi watoke katika ile nchi walikokuwa na waingie katika nchi ya ahadi, kabla Masihi wao aliyeahidiwa hajaja.

Na inabidi Kanisa lifanye kitu kile kile. Watoke kwenye lile kundi la wakanaji na kwenda kwenye Ahadi, kabla Masihi hajadhihirishwa mbele yao. Mnaliona hilo? Uzima wa Masihi uliodhihirishwa kuliandaa Kanisa, Bibi Mwanamke huolewa na mwanamume na kutopatana naye, itakuwa namna ya fujo siku zote. Lakini mume na mke wake, mpenzi wake, huyo aliyemposa, wanapokuwa katika amani kamilifu, kama nafsi moja na nia moja, kwa sababu wanakwenda kuwa mwili mmoja. Basi Kanisa linapokuwa katika amani kama hiyo na Mungu hadi udhihirisho wa Bwana Arusi unadhihirishwa katika Bibi Arusi, kwa sababu wanakwenda kuwa Mmoja. Ama, ni somo kuu mno. Vema. Vema, sasa kumbukeni, akili za kiroho zikichukua hili zinaweza kuona mfano na kinyume cha mfano na kuchukua moja. Tungeweza kuendelea kwa masaa juu yake. Tazama kile kinachotokea.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Kutoka kwa Tatu.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Forerunner.

Jina la Mungu.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni apple?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

  Maandiko Anasema...

Haya basi, nitakutuma sasa kwa Farao, ili upate kuwatoa watu wangu, hao wana wa Israeli, katika Misri.

Musa akamwambia Mungu, Mimi ni nani hata niende kwa Farao nikawatoe Wana wa Israeli watoke Misri?

Akasema, bila shaka mimi nitakuwa pamoja nawe; na dalili ya kuwa nimekutuma ndiyo hii; utakapokuwa umekwisha kuwatoa hao watu katika Misri, mtamwabudu Mungu katika mlima huu.

Kutoka 3:10-12


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDF Kiingereza)
 

Chapter 11
- The Cloud

(PDF Kiingereza)
 

William Branham Life
Story.

(PDF Kiingereza)

How the Angel came
to me.
(PDF Kiingereza)

Ni wakati wa
kutoka. Ni wakati
wa kuitwa nje
kwenda Nchi
ya Ahadi...
Utawala wa Miaka
Elfu Moja.



Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.