Kusudi la Mungu.

<< uliopita

ijayo >>

  Neno lililo hai mfululizo.

Kristo ni siri ya Mungu iliyofunuliwa.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Kristo ni siri ya Mungu iliyofunuliwa.

Angalia, Mungu alikuwa na kusudi lenye awamu tatu katika hili fumbo la siri kuu. Mungu, katika fumbo la siri Yake kuu ile aliyokuwa nayo kabla ulimwengu haujaanza, Yeye alikuwa na kusudi lenye awamu tatu ndani yake. Na sasa kile tunachotaka kukiendea asubuhi hii ni hilo kusudi lenye awamu tatu ni nini? Sasa naamini, kwa msaada wa Mungu, Ambaye yupo hapa na Yeye -atatuonyesha hilo. Sasa, ikiwa Yeye alikuwa na kusudi lenye awamu tatu tunataka kujua hilo kusudi lenye awamu tatu ni nini.

Jambo la kwanza lilikuwa, kwamba Mungu alitaka kujifunua Mwenyewe kwa watu. Yeye asingeweza kulifanya kama Yehova Mungu mkuu Ambaye amefunika anga lote, wakati, na Umilele wote. Asingeweza kufanya Yeye ni mkuu mno kuweza kufunuliwa kwa watu, kwa sababu ingekuwa ya kimiujiza kupindukia. Jinsi gani kile Kiumbe kikuu ambacho hakikuwa na mwanzo... ambapo ukishatoka nje ya mzunguko wa mamia ya mabilioni na matrilioni na matrilioni ya karne za anga na kuingia kusikokuwa na mwisho, ndani ya Umilele, na Kiumbe mkuu namna hii. Aliyekuwa vyote hivyo na hivyo ndivyo alivyo hadi leo.

Lakini kile Yeye alichotaka kufanya, Yeye alipenda Ubaba, kwani Yeye alikuwa Baba. Na njia pekee ambayo Yeye angejidhihirisha ilikuwa ni kuwa Mwana wa Adamu. Hiyo ndiyo sababu Yesu alidumu kusema “Mwana wa Adamu”. Unaona, hawakujua kile Yeye alichokuwa akiongelea, wengi wao. Lakini sasa mnalielewa? Unaona? Yeye alitaka kujidhihirisha Mwenyewe. Hilo lilikuwa Lake, mojawapo ya awamu tatu za kusudi Lake ilikuwa ni kujidhihirisha Mwenyewe katika Kristo.

La pili, kuchukua nafasi ya utangulizi katika Mwili Wake wa waamini, yaani Bibi arusi Wake, ili kwamba Yeye aweze kuishi ndani ya watu.

Sasa, Yeye angeweza kufanya hilo ndani ya Adamu na Hawa, lakini dhambi iliwatenganisha, kwa hiyo sasa ingepasa njia fulani kulirudisha tena. Ee, jamani! Ee, sasa, hili, hili ni jambo la kina kwangu, hata kule kulifikiria tu. Unaona? Unaona kusudi la Mungu lilikuwa nini? Sasa kwa nini Yeye hakuwaacha Adamu na Hawa vile? Basi Yeye kamwe asingeweza kuonyesha utimilifu Wake., tabia Yake kikamilifu. Kwa sababu, Yeye angeweza kuwa Baba pale, hiyo ni kweli, lakini Yeye ni Mwokozi vile vile. Unasema “Unajuaje Yeye alikuwa hivyo?” Yeye ni hivyo, kwa sababu nimekuwa na ushirika Naye. Unaona? Yeye ni Mkombozi, na ilipasa adhihirishe hilo. Na angelifanya hilo vipi? Kwa kupitia Kristo pekee. Angewezaje kuwa Mwana? Kupitia Kristo tu Angewezaje kuwa Mponyaji? Kwa kupitia Kristo tu. Unaona, vitu vyote vimekamilishwa katika yule Mtu mmoja, Yesu Kristo. Lo, jamani!

Ninapoliwazia na-naona tu madhehebu yalipita na kutokomea na kila kitu kingine vikienda tu, unaona mnapoona kusudi kuu la Mungu akijifunua Mwenyewe. Na kwanza ikiwa ni kule kujifunua Mwenyewe katika Kristo, “utimilifu wa Uungu katika mwili.” Na kisha kuuleta “utimilifu wa Uungu katika mwili” ndani ya watu ili aweze kuchukuea nafasi ya utangulizi, usimamizi wa uongozi.

Usiku ule mwingine mmoja, kama hukupata ile kanda, nilihubiri hapa jioni moja, juu ya Mfungwa wa Yesu Kristo. Paulo, mtumwa. Unaona? Mungu anapokufanya kuwa mtumwa Wake, basi huwezi kufanya chochote ila kile Roho anachosema ufanye. Paulo, pamoja na akili zake nyingi, alifundisha... alifundishwa na Gamalieli kuwa kuhani mkubwa au rabi, siku moja. Naye alikuwa na matazamio makubwa. Kiakili alikuwa mtu mkuu katika taifa. Lakini ilipasa atoe kila kimoja cha hayo mhanga, unaona, awe sehemu ya Neno, kumdhihirisha Yesu Kristo. Yeye alijua ilikuwa ni nini kusema... Alikuwa na wazo la kwenda mahali fulani, ndugu fulani walikuwa wamemwita, lakini alikatazwa na Roho kufanya mapenzi yake mwenyewe. Ee, laiti-laiti watu wa kiroho nusu wanaweza kuchukua hilo! Unaona? Alikatazwa kufanya mapenzi yake mwenyewe. Angeweza tu kufanya... “Roho alinikataza.” Unaona? Yeye alikuwa mfungwa wa Kristo.

Ndipo, huyo mpiga ramli siku moja, ambaye yeye Paulo alijua alikuwa na uwezo wa kutoa yule pepo, lakini angeweza tu kufanya hivyo jinsi Mungu alivyotaka. Siku kwa siku alimfuata, akimlilia, lakini siku moja Roho alimpa ruhusa. Ndipo akamkemea yule msichana ile roho iliyokuwa ndani yake. Unaona? Yeye alijua kuwa mfungwa ilikuwa ni nini.

Musa, akili zake, ingepasa azipoteze ili kumpata Kristo, kuwa mfungwa. Basi Mungu alipouondoa ulimwengu wote ndani yake, na uwezo wote aliokuwa nao, na kusimama kwenye Uwepo wa ile Nguzo ya Moto siku ile alishindwa kusema. Hakuweza hata, alisema hakuweza hata kuongea. Basi hapo Mungu alikuwa na mtumwa. Unaona? Huwezi kujaribu kwa uchunguzi wako mwenyewe. Basi Mungu ilimpasa amjalie huyu mtu, kumjalia nguvu ya kutosha ili kwamba weze kwenda chini kule.

Naye akasema, “Bwana, nilimwambia Farao kile Wewe ulichosema naye hakufanya.”
Akasema, “Basi chukua hii fimbo yako.” Mungu akinena, hilo ni Neno la Mungu, “nenda kule na uielekeze Mashariki, na uite inzi.” Na mainzi yakaumbika, kwa sababu Yeye alikuwa na mfungwa ambaye Farao asingeweza kumlipa mshahara kwa chochote. Hakuna mtu mwingine yeyote angeweza kumgeuza aelekee kwingine. Yeye alikuwa mtumwa kamili katika minyororo ya Neno la Mungu aliyekuwa amefungwa kutii tu HIVI ASEMA BWANA.

Ee, ikiwa Mungu anaweza kujipatia watumwa wa aina hiyo! Sasa, hiyo ni wakati Yeye anaweza kudhihirisha nafasi Yake ya utangulizi, unaona? Yeye, Yeye ana mtu, au mtu, ambaye kwamba hajui chochote ila Kristo. Mnalipata ninalomaanisha? Vema. Hilo ni la pili. Kwanza, kujidhihirisha kabisa Mwenyewe, Mungu katika Kristo. Pili, kuchukua nafasi ya utangulizi, kwa hili, katika Kanisa Lake, ambalo ni Mwili Wake, Bibi arusi, mpaka Yeye awe mtangulizi ajidhihirishe Mwenyewe kupitia kwao. Vema.

Na, tatu, kurejesha Ufalme mahali pake panapostahili, ule ulioanguka kwa kwa dhambi kwa a jia ya Adamu wa kwanza, hadi kurejea kule nyuma wakati Yeye alipotembea jioni wakati wa kupunga kwa jua, pamoja na watu Wake, akaongea nao akawa na ushirika nao. Na sasa dhambi na kifo vimewatenganisha na Uwepo na udhihirisho Wake wote. Je, mnalisoma? Kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu kudhihirisha tabia zake zote, kile Yeye alichokuwa.

Kwa hiyo, ikiwa Mwamini wa Utatu yeyote hapa angejiachia kwa dakika, unaweza kuona kuwa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu si Miungu watatu. Ni sifa tatu za Mungu yule yule. Unaona, ni udhihirisho. Yeye alikuwa Baba alitaka kuwa Baba. Yeye alikuwa Baba, Yeye alikuwa Mwana, na Yeye ni Roho Mtakatifu. Na Baba na Roho Mtakatifu ni Roho yule yule. Je, hamwoni? Mnalielewa? Siyo miungu watatu. Mashetani walikuambia vitu hivyo, kuwafanya muabudu sanamu. Unaona? Ni Mungu mmoja akielezwa katika sifa tatu. Kuwa Baba, kuwa Mwokozi, kuwa Mwana, kuwa Mponyaji, unaona ni madhihirisho Yake.

Nataka kuendelea kwa ulaini kwa muda kidogo tu ili kwamba hata watu wanaosikiliza kanda wataweza kupata hilo wazo, wale wawezao kuona. Ingenichukua mzunguko mzima wa saa, siku nzima, kuelezea moja tu ya masomo hayo. Lakini nadhani nalifanya dhahiri vya kutosha kiasi kwamba unaweza kuona kile ninachokiendea. Unaona?

Mungu, aliyejidhihirisha katika Yesu Kristo, Ambaye alikuwa yote, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, “utimilifu wa Uungu katika mwili”. Sasa, “utimilifu wote wa Uungu katika mwili” unakaa katika Kanisa Lake, nafasi ya utangulizi wote. Yote yale Mungu aliyokuwa, Yeye aliyamwaga kwa Kristo; na yote aliyokuwa Kristo, yalimwagwa katika Kanisa, waamini. Si dhehebu! Tutafikia hilo katika dakika chache, na italiondoa kutoka akilini mwako daima, unaona, kukuonyesha kinachosababisha hilo, kwa msaada wa Mungu, kama Yeye ataliruhusu lije kwetu.

Kusudi lake ni nini Sasa? Kujidhihirisha Mwenyewe kama Mwana, unaona, na, sasa ndani Yake ungekaa, “Utimilifu wa Uungu katika mwili.” Nina Wakolosai imekaa hapa, mbele yangu hapa hapa. Unaona? Kwamba, katika Andiko lote, hilo ndilo lilikuwa kusudi la Mungu. Ndipo, na kupitia huu uzima wa huyu Mwana, msalaba wake, “ile Damu,” linasema hapa, “ya msalaba Wake,” kwamba aweze kujipatanishia na nafsi Yake Mwenyewe Mwili, Bibi arusi: ambaye ni Hawa, Hawa wa pili. Na Mungu hulitoa katika mfano, kama alivyofanya kwa Musa na wote. Jambo lile lile alilofanya katika Adamu na Hawa, akatoa mfano, kuwa walikuwa Kristo na Bibi arusi. Yeye ni Adamu wa pili; Kanisa ni Hawa wa pili.

Na kadiri Hawa wa pili anavyofanya suluhu dhidi ya Neno, je, hafanyi jambo lile lile alilofanya Hawa wa Kwanza? [Kusanyiko linasema “Amina”Mh]. Akijaribu kusema, “Vema, ilikuwa kwa ajili ya kipindi kingine.” Na tutalifikia hilo katika dakika chache zijazo, ikiwa Yeye alisema ilikuwa kwa ajili ya kipindi kingine. Itakuwaje kipindi kingine wakati Yeye ni Yeye “yule jana, leo, na hata milele?” Lakini Mungu alilikusudia hilo na “kulificha machoni pa wenye busara na hekima na kuwafunulia watoto waliochaguliwa kimbele” ambao walichaguliwa kimbele kulipokea.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Kristo ni siri ya Mungu iliyofunuliwa.



Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Forerunner.

Jina la Mungu.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni apple?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

  Maandiko Anasema...

Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo.

Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.

1 Wakorintho 12:12-13


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDF Kiingereza)

Marriage and Divorce.

(PDF Kiingereza)

William Branham Life
Story.

(PDF Kiingereza)

How the Angel came
to me.
(PDF Kiingereza)