Nguvu ya Mungu ya kubadilisha umbo.

<< uliopita

ijayo >>

  Neno lililo hai mfululizo.

Kufanywa upya nia zenu.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Nguvu ya Mungu ya kubadilisha umbo.

Sasa pale katika Kitabu cha Warumi, ile sura ya 12, na ile aya ya 1 na ya 2 tunataka-tunatakai kusoma hili Andiko.

Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.
Wala msiifuatilishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.

Sasa, Bwana akipenda, nataka kuchukua somo langu kwa ajili ya asubuhi hii, juu ya Nguvu ya Mungu ya Kubadilisha Umbo. Kwamba msifuatilishe namna ya dunia hii.: bali... mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, sasa, na mpate kujua hakika yale ambayo ni mapenzi ya Mungu yaliyo mema, makamilifu na ya kumpendeza.

Ni fungu la maneno la zamani lililozoeleka ambalo wengi wa wachungaji wenu wamelitumia wakati wote ambao mmekuwa nao. Limekuwa likitumika tangu liandikwe. Lakini bado, jambo moja kuhusu Neno la Mungu, kamwe halizeeki, kwa sababu ni Mungu. Kamwe halizeeki. Kupitia kila kizazi sasa, kwa karibu kabisa, kwenye miaka elfu mbili na mia nane, au zaidi, hili Neno la Mungu limekuwa likisomwa na watu, makuhani, na kadhalika, na kamwe halizeeki. Mimi mwenyewe, nimekuwa nikilisoma Hili, kwa miaka thelathini na tano. Na kila wakati ninapolisoma, ninakuta kitu fulani kipya ambacho nilikiruka mara ya kwanza. Kwa sababu, limevuviwa, ni Mungu katika umbo la herufi. Unaona, ni sifa za Mungu zikiendelea kunena,na kuwekwa kwenye karatasi.

Mara nyingi, mtu alisema, “Vema, sasa, watu waliandika hii Biblia.” Hapana. Biblia inasema, Yenyewe, kwamba Mungu aliandika Biblia. Ni Neno la Mungu. Na kamwe halitaweza kushindwa. Yesu alisema, “Mbingu na nchi zitashindwa, zitapita, lakini Maneno Yangu hayatashindwa kamwe.” Na haliwezi kushindwa, na likiwa Mungu, kwa sababu ni sehemu Yake. Na ndipo wewe ukiwa mwana na binti, wewe ni sehemu ya Hilo, na hilo hukufanya sehemu Yake Yeye. Hivyo ndiyo sababu tunakuja kushiriki pamoja kwenye Neno la Mungu.

Sasa hili neno kilichobadilishwa umbo nilitazama katika kamusi, jana, wakati karibu nishindwe kufuatia muda ambao ilipasa niwe juu hapa, nilipokuwa nikitafuta mada ya kuhubiria, na nikapata hili neno, au mada hii ya kuhubiria, namaanisha, Andiko. Na katika kamusi inasema kwamba ni “kitu fulani kilichobadilishwa.” Inapasa “kubadilishwa.” Kilichobadilishwa umbo, “kimefanywa tofauti na kilivyokuwa.” Kimekuwa, “Tabia yake na kila kitu kimebadilishwa ndani yake,” kubadilisha umbo.

Na nikifikiri asubuhi hii, katika Mwanzo 1. Huu ulimwengu haukuwa na umbo, na ulikuwa utupu, na giza lilikuwa juu ya nchi; hakuna chochote ila vurugu tupu. Na huu ulimwengu ulipokuwa katika ile hali, Roho wa Mungu alitembea juu ya uso wa maji, na picha yote ilibadilishwa, kutoka kwenye vurugu tupu, kuwa bustani ya Edeni. Hiyo ni Nguvu ya Mungu ya ianyobadilisha umbo, ambayo inaweza kuchukua kitu fulani ambacho si chochote na kukifanya kitu fulani kizuri katika kutokana na hicho. Nguvu ya Mungu ya inayobadilisha umbo!

Na tunafahamu kuwa, kwa-kwa kusoma Maandiko, kwamba Mungu alikuwa kwa miaka elfu sita akifanya maandalizi haya kwa ajili ya hii Edeni. Sasa, Yeye anaweza kuwa hakuchukua muda mrefu hivyo; ila tukitazamia tu, na kulichukua hili kutoka kwenye Andiko pale liliposema, “siku moja kwa Mungu, ni miaka elfu moja duniani,” yaani, ikiwa Mungu angehesabu muda. Na kusema ilikuwa miaka elfu sita aliyokuwa nayo Yeye katika kuumba dunia, na Yeye alikuwa ameotesha juu ya nchi mbegu nzuri zote. Hapo kulikuwa tu na kila kitu kikamilifu. Nafikiri, mara nyingi, wakati hata wakosoaji wanapoanza kusoma Kitabu cha Mwanzo, wanaanza kukikosoa, kwa sababu inaonekana kama kinaendelea kujirudia Chenyewe, au kinakutupa nje hapa na pale. Lakini ikiwa tungeona kwa kitambo kidogo, kabla hatujaingia katika somo letu, kuwa, kuwa Musa aliona ono. Na Mungu alinena naye. Mungu alinena na Musa uso kwa uso, mdomo kwa sikio. Sasa, Yeye kamwe hakunena kwa mtu mwingine namna hiyo, kama Yeye alivyofanya kwa Musa. Sasa, Musa alikuwa mkuu, mmoja wa manabii wakuu zaidi ya wote. Alikuwa mfano wa Kristo. Na sasa Mungu anaweza kunena, Yeye ana sauti. Imesikika. Mungu anaweza kunena.

Na Mungu anaweza kuandika. Mungu aliandika zile Amri kumi kwa kidole Chake Mwenyewe. Aliandika juu ya kuta za-za Babeli zamani, kwa kidole Chake. Yeye aliinama chini na kuandika mchangani wakati mmoja, kwa kidole Chake. Mungu anaweza kunena. Mungu anaweza kusoma. Mungu anaweza kuandika. Mungu ndiye Chemchemi ya neema yote na Uwezo, na Hekima yote ya Kiungu, iko ndani ya Mungu. Hivyo basi, tukijua kuwa, Yeye Ndiye pekee Muumbaji aliyeko. Hakuna Muumbaji mwingine isipokuwa Mungu. Shetani hawezi kuumba, kamwe, yeye hupotosha tu kile kilichokwishaumbwa tayari. Lakini Mungu Ndiye pekee aliye Muumbaji. Kwa hiyo, Yeye aliumba kwa Neno Lake. Yeye alituma Neno Lake. Kwa hiyo mbegu zote ambazo Yeye aliziweka juu ya nchi, Yeye aliumba zile mbegu kwa Neno Lake Mwenyewe, kwani hakukuwa na chochote kingine ambacho mbegu zingefanyizwa kutokana nacho. Yeye aliziweka, na zilikuwa chini ya maji. Yeye alisema tu, “Kuwe na hiki, na kuwe na kile.

Sasa tunakuta kuwa, mara nyingi, inaonekana kama Biblia inarudia au inasema kitu fulani kwa kitu ambacho haikisemi. Kwa mfano, katika Mwanzo 1 tunakuta kuwa, “Mungu aliumba mtu kwa mfano Wake Mwenyewe, kwa mfano wa Mungu Yeye alimuumba; mwanamume na mwanamke Yeye aliwaumba.” Na ndipo Yeye anaendelea, na mambo mengi yalitukia juu ya dunia. Ndipo tunakuja kukuta hakukuwa na mtu wa kuilima ardhi. “Ndipo Mungu akaumba mtu kutoka kwenye vumbi la nchi.” Huyo alikuwa mtu tofauti. “Naye akapulizia pumzi ya uzima ndani mwake, naye akawa nafsi iliyo hai.”

Mtu wa kwanza alikuwa katika mfano wa Mungu, ambao ni Roho. Yohana 4 , anasema, “Mungu ni Roho, na wale wamwabuduo Yeye lazima wamwabudu katika Roho na Kweli.” Lakini Mungu ni Roho. Na mtu wa kwanza ambaye Yeye alimuumba, alikuwa mtu wa roho, naye alikuwa katika mfano na mwenye kufanana na Mungu. Na ndipo akamweka huyu mtu katika nyama, na yule mtu akaanguka. Hivyo ndipo Mungu akashuka na kuwa mfano wa mtu, kwamba Yeye aweze kumkomboa yule mtu aliyeanguka. Hiyo ndiyo habari halisi ya Injili, kwa-kwa maoni yangu.

Sasa, Mungu, katika miaka elfu sita, alikuwa amepanda hizi mbegu nzuri zote, au Yeye alikuwa amenena Neno Lake. “Itakuwa hivi. Huu mti utakuwepo. Hii itakuwepo.” Kila kitu kilikuwa kikamilifu. Kilikuwa kizuri tu. Na Yeye akaamuru kila moja ya zile mbegu kwamba zingekuwepo, zingejibadilisha zenyewe kuwa mmea wa namna fulani ya uzima ambao lile Neno la Mungu limenena ndani yake ziwe. Ikiwa ilikuwa mti mwaloni, ulikuwa uzae mti mwaloni. Ikiwa ulikuwa mchikichi, ulikuwa uzae mawese. Kwa sababu, yule Muumba mkuu alikuwa tu, alituma Neno Lake, na Neno mbegu lilikuwa pale kabla mbegu halisi haijafanywa. Na Neno lilifanyiza mbegu. Unaona, “Yeye aliumba ulimwengu kutokana na vitu visivyoonekana.” Unaona, Yeye-Yeye aliumba ulimwengu kwa Neno Lake. Mungu alinena kila kitu kikawepo.

Naye akiwa Mungu, Muumba, akinena kila kitu na kikaweko, lazima ulikuwa ulimwengu mkamilifu. Palikuwa-mahali pazuri. Ilikuwa paradiso halisi isiyoghoshiwa hapa duniani. Sasa, kama, kila mahali inavyopasa pawe na makao makuu mahali fulani. Huu mkutano wa kiroho una makao makuu, na mkutano huu wa wahudumu una makao makuu, na kanisa lina makao makuu. Na Mungu ana makao makuu. Na hivyo hii sehemu kuu, taifa tunaloishi ndani yake, lina makao makuu. Na hivyo hii Edeni kuu ilkuwa na makao makuu, na makao yake makuu yalikuwa na kinara chake katika bustani ya Edeni, au katika Edeni, mashariki mwa bustani. Na Mungu alimweka Mwana Wake na Bibi arusi wa Mwanawe, Adamu na Hawa, juu ya haya, watawale maumbile Yake makuu yote hapa duniani.

Na Mungu alikuwa Baba wa Adamu. “Adamu alikuwa mwana wa Mungu,” kulingana na Maandiko. Yeye alikuwa mwana wa Mungu. Na Mungu akamfanyia msaidizi, kutoka kwenye mwili wake mwenyewe; labda ubavu kutoka juu ya moyo wake, ili huyo awe karibu naye, na akamfanyia msaidizi. Ilikuwa bado huyu kuwa mke wake kwa kweli, kama ambavyo ilikuwa yeye ni mtu bado; Mungu alikuwa amelinena tu mara. Na pale ndipo tatizo lilipokuja, Shetani alimpata kabla ya Adamu kumpata. Kwa hiyo, lilikuwa tu Neno Lake alilokuwa amenena.

-----
Na bado sisi sote tuko katika mfano wa Mungu. Lakini baadhi wamekwishaumbuliwa mno, kama wana wa Mungu, wale wanaotembea kinyume cha Neno Lake na njia Yake ile-ile aliyotuweka sisi na kuiandaa kwa ajili yetu sisi kutembea humo. Akiweka jambo fulani, ulimwengu hutupindisha kututoa njiani, unatuvuta zaidi karibu nao, na mbali na ile njia iliyonyooka, nyembamba Yeye aliyotupanda ndani yake, kuwa wana na binti za Mungu. Dhambi imefanya hili jambo ovu kwa wana na mabinti wa Mungu.

-----
Sasa kwenu ninyi mnaosikiliza kutoka hewani, popote mlipo, nawataka ninyi mumpokee Kristo nje kule, kama Mwokozi wako binafsi, na mjazwe kwa Roho Wake. Yale maneno yaliyosemwa aubuhi hii, hebu yadondoke mioyoni mwenu. Na hebu mumpokee Yesu kule. Na mtazame maisha yenu, na muone kile mtakachoishi baadaye. Na mchukue Chujio la mtu mwenye akili hapa. Unapojiona mwenyewe ukifanya jambo fulani lililo kinyume na hili Neno, ondoka kwenye hilo, haraka kabisa. Unaona? Kwa sababu, kuna Chujio linaloweka kifo mbali na wewe, hilo ni Neno la Mungu. Maneno Yake ni Uzima, na yatakuepusha na kifo.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Nguvu ya Mungu ya kubadilisha umbo.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Forerunner.

Jina la Mungu.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni apple?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

  Maandiko Anasema...

Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.

Mwanzo 1:2


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDF Kiingereza)

Marriage and Divorce.

(PDF Kiingereza)

William Branham Life
Story.

(PDF Kiingereza)

How the Angel came
to me.
(PDF Kiingereza)


Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.