Muhuri Wa Kwanza.

<< uliopita

ijayo >>

  Mihuri Saba mfululizo.

Farasi nyeupe mpanda farasi.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Muhuri Wa Kwanza.

Sasa, katika sura hii ya 5, kule kuvunjwa kwa Mihuri hii, na sasa kile Kitabu kilichotiwa Mihuri Saba. Kwanza, tunataka kusoma Muhuri wa Kwanza. Jana jioni, ili kuliweka misingi kidogo zaidi, tunatambua, ya kwamba, Yohana alipotazama na kukiona kile Kitabu kingali kiko mikononi mwa Mwenyewe wa asili, Mungu. Je, mnakumbuka vile kilivyopotezwa? Na Adamu. Yeye alipoteza kile Kitabu cha Uzima, kwa kupenda maarifa ya Shetani, naye akapoteza urithi wake, akapoteza kila kitu; na hakuna njia ya kupata Ukombozi.

Ndipo, Mungu, akifanyika mfano wa mwanadamu, akashuka na akawa Mkombozi kwetu, apate kutukomboa. Na sasa tunaona ya kwamba, katika siku zilizopita, mambo haya yaliyokuwa siri yatafunuliwa kwetu katika siku hizi za mwisho.

Sasa tunaona, pia, katika jambo hili, ya kwamba, mara tu Yohana aliposikia tangazo hili la-la kuja kwa Mkombozi aliye Jamaa wa Karibu na kufanya madai yake, hapakuwa na mtu ambaye angeweza kufanya jambo hilo; hakuna mtu Mbinguni, hakuna mtu duniani, hakuna mtu chini ya nchi. Hakuna yeyote aliyestahili hata kukitazama Kitabu kile. Hebu wazia tu jambo hilo. Hakuna mtu, kabisa, aliyestahili hata kukitazama. Na Yohana akaanza tu kulia.

Yeye alijua ya kwamba, loo, hakukuwako sasa na nafasi ya ukombozi. Kila kitu kimeshindwa. Na mara moja tunaona kulia kwake kukikoma, upesi, kwa sababu ilitangazwa na mmoja wa hao Wenye Uhai wanne, ama wazee, ndiyo namaanisha. Mmojawapo wa-wa wazee akasema, “Usilie, Yohana, kwa maana Simba aliye wa kabila la Yuda ameshinda,” yaani, “ametiisha, na amepata ushindi.”

Yohana, alipogeuka, akamwona Mwanakondoo akitokea. Lazima alikuwa amelowa damu na amekatwa na kujeruhiwa. Alikuwa amechinjwa, ninii...ilisema, ya kwamba, “Mwanakondoo aliyechinjwa.” Na, bila shaka, alikuwa bado anatoka damu; kama ulipata kumchinja mwanakondoo na-na kumwua jinsi huyo Mwanakondoo alivyouawa, na hata hivyo. Alikuwa amekatwa vipande-vipande msalabani, mikuki ubavuni, na misumari mikononi na miguuni, na miiba juu ya paji la uso. Alikuwa katika hali mbaya sana. Na Mwanakondoo huyu akaja, akamwendea Yeye aliyeketi juu ya kile Kiti cha Enzi, aliyeshikilia hati miliki yote ya Ukombozi. Na Mwanakondoo anaondoka anakwenda na kukitwaa Kitabu toka kwenye mkono Wake Yeye aliyeketi juu ya Kile Kiti cha Enzi, na kukichukua, na kufungua ile Mihuri na kukifungua kile Kitabu.

Na basi jambo hilo lilipotendeka, tuliona kwamba lazima kulikuwako na kitu fulani kikuu kilichotendeka Mbinguni. Kwa maana, wale wazee, na wale wazee ishirini na wanne, na wale wenye Uhai, na-na kila kitu Mbinguni, kilianza kupaza sauti, “Umestahili!” Baadaye hawa hapa Malaika wanakuja, na kumwaga vitasa vya maombi ya watakatifu. Wale watakatifu waliokuwa chini ya madhabahu wakapaza sauti, “Umestahili, Ewe Mwanakondoo, kwa kuwa umetukomboa, na sasa umetufanya wafalme na makuhani, nasi tutatawala juu ya nchi.” Loo, jamani! Na hiyo ndivyo ilivyo, hapo Yeye alipokifungua kile Kitabu.

Unaona, Kitabu chenyewe hasa kilipangwa na kuandikwa kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Kitabu hiki, Biblia, hasa kiliandikwa kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Na Kristo, akiwa yule Mwanakondoo alichinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. nao wa-washiriki wa Bibiarusi Wake, majina yao yaliwekwa katika Kitabu cha Uzima cha Mwanakondoo kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Lakini, kimetiwa muhuri, na sasa hivi kinafunuliwa; ni akina nani majina yao yalikuwa humo ndani, mambo yanayokihusu, na ni jambo kuu kiasi gani! Naye Yohana, alipokiona, a-alisema, “Kila kitu Mbinguni, kila kitu chini ya nchi....” Kila kitu kilimsikia akisema, “Amina, baraka, na heshima!” Yeye kweli alikuwa na furaha kuu, na, kwa kuwa, “Yule Mwanakondoo alistahili.”

Na sasa Mwanakondoo amesimama. Sasa, usiku wa leo, tunapoingia sura hii ya 6, Yeye ana kile Kitabu mkononi Mwake, na anaanza kukifunua. Na, loo, ningeninii kabisa leo...Na natumaini kuwa watu ni wa kiroho. Ningefanya kosa baya sana katika jambo Hilo, kama haingekuwa, yapata saa sita leo, wakati Roho Mtakatifu alipokuja chumbani na kunisahihisha kuhusu jambo fulani nililokuwa nikiandika nije niseme. Nilikuwa nikilichukua kutoka katika somo la siku nyingi. Sikuwa na chochote juu ya jambo Hilo. Sijui Muhuri wa Pili ni nini, hata kidogo. Lakini nilikuwa na somo la kitu cha zamani cha yale niliyokuwa nimehubiri miaka kadhaa iliyopita, basi nikaandika hilo.

Nami nilikuwa nimekusanya somo hili, somo kutoka kwa Dk.Smith, walimu wengi wakuu, mashuhuri ambao nili-nilikuwa nimelichukua kutoka kwao. Nao wote waliamini jambo hilo, kwa hiyo nilikuwa nimeliandika. Nami nilikuwa ninajiandaa kusema, “Vema, sasa nitalisoma kutokana na msimamo huo.” Na hapo, yapata saa sita mchana, Roho Mtakatifu alishuka tu kwa ghafla moja kwa moja chumbani, na jambo lote zima likafunguka tu kwangu, na likawa ndio hilo hapo, unaona, kuhusu huu-kuhusu huku kufunguliwa kwa Muhuri huu wa Kwanza.

Nina hakika kama nilivyosimama hapa usiku wa leo, ya kwamba haya nitakayosema hapa ni Kweli ya Injili. Na-najua tu ni Ukweli. Kwa sababu, kama ufunuo uko kinyume na Neno, basi si Ufunuo. Na, ninyi mnajua, kuna mambo mengine yanayoweza kuonekana kama ni kweli kabisa, na hali si kweli. Unaona? Yanaonekana kama ni ya kweli, bali si kweli.

Sasa, tunamwona, Mwanakondoo akiwa na Kitabu, sasa. Na sasa katika sura ya sita tunaona.

1 Kisha nikaona hapo Mwanakondoo alipofungua moja ya zile mihuri saba, nami nikasikia mmoja wa wale wenye uhai wa nne akisema, kama kwa sauti ya ngurumo, Njoo uone.
2 Nikaona, na tazama farasi mweupe, na yeye aliyempanda ana uta, akipewa taji, naye akatoka, ali akishinda tena apate kushinda.

Sasa, huo ndio Muhuri wa Kwanza, ule ambao tutajaribu, kwa neema ya Mungu, kuuelezea usiku huu. Iwezekanavyo kabisa...Nami natambua ya kwamba mtu, akijaribu kuuelezea Huo, hua anatembea hatarini kama hujui unachofanya. Kwa hiyo kama likinijia kwa Ufunuo, nitawaambia hilo. Kama itanibidi kulitoa katika mawazoni mwangu, basi nita-nitawaambieni hilo kabla sijanena habari zake. Lakini nina hakika kabisa, kama ninavyosimama hapa usikuwa leo, Huo ulinijia mpya, leo, kutoka kwa Mwenyenzi. Sivutiwi kujisemea mambo kama hayo vyo vyote tu, tunaponena kuhusu sehemu hii ya Maandiko. Nina-ninatumaini... Ninatumaini mnajua kile ninachozungumzia sasa, mnaona. Basi, mnajua, huwezi kusema mambo...Kama kitu fulani kinapaswa kiwe kimekaa hapa kabla hakijatendeka, hu-huwezi kusema jambo hilo mpaka kitu fulani kikiweke pale. Unaona? Mnasoma? Hivi mnasikiliza jambo fulani? Unaona?

Sasa, ile gombo la Kitabu cha Muhuri Saba, sasa linafunguliwa na Mwanakondoo. Tunapaendea mahali hapo usiku wa leo. Mungu, na atusaidie. Wakati Mihuri hii inapovunjwa na kufunguliwa, siri za hicho Kitabu zinafunuliwa. Sasa, unaona, Hiki ni Kitabu kilichotiwa mihuri. Sasa, tunaamini jambo hilo. Sivyo? [kusanyiko linasema, “Amina.”-Mh.] Tunaamini ya kwamba ni Kitabu kilichotiwa muhuri. Sasa, hatukujua jambo hilo hapo nyuma, lakini kimetiwa muhuri. Kimetiwa muhuri kwa Mihuri Saba. Hiyo ni kusema, upande wa nyuma wa hicho Kitabu, kimetiwa muhuru kwa Mihuri Saba.

Kama tungalikuwa tukiongelea juu ya kitabu cha namna hii ingekuwa ni kama kukizungushia ukanda, mikanda saba. [Ndugu Branham anaonyesha kitabu cha mfano- Mh.] Lakini si kitabu cha aina hii. Ni kitabu cha hati iliyokunjwa. Na ndipo basi gombo hilo lilipokunjuliwa, huo ni mmoja; halafu humo ndani ya gombo hilo ni wa pili. Na papa hapa inasema huo ni nini, lakini ni siri. Lakini, hata hivyo, tumeichunguza-chunguza humo ndani, lakini, kumbukeni, hicho Kitabu kimetiwa muhuri. Na Kitabu hicho ni Kitabu cha siri, ya Ufunuo. Ni ufunuo wa Yesu Kristo, unaona, Kitabu cha Mafunuo. Na sasa mnajua, Huko nyuma kote katika wakati, mwanadamu amechunguzachunguza na kujaribu kuingilia jambo Hilo. Sote tumefanya hivyo.

-----
Ndipo, hapo Mwanakondoo alipochukua kile Kitabu na kuvunja huo Muhuri wa Kwanza, Mungu alinena kutoka katika Kiti Chake cha Enzi cha Milele, kusema huo Muhuri ulikuwa na kitu gani, cha kufunuliwa. Lakini ulipowekwa mbele ya Yohana, ulikuwa katika mfano. Yohana alipouona, ulikuwa bado ni siri. Kwa nini? Haikuwa hata umefunuliwa wakati huo. Hauwezi kufunuliwa mpaka yale Yeye aliyosema hapa, “penyea wakati wa mwisho.” Lakini ulikuwa katika mfano.

Wakati, ile “iliponguruma.” Kumbukeni, sauti kuu ya kishindo cha Ngurumo ni Sauti ya Mungu. Hiyo ndiyo Biblia isemavyo, unaona, “kishindo cha Ngurumo.” Wao walidhani ilikuwa ni ngurumo, lakini ilikuwa ni Mungu. Yeye aliielewa, kwa maana ilifunuliwa kwake. Unaona? Ilikuwa ni Ngurumo. Na, angalia, Muhuri wa Kwanza ulifunguliwa. Muhuri wa kwanza, wakati ulipofunguliwa katika mfano, ilinguruma. Sasa je! Ni vipi utakapofunguliwa katika hali yake halisi?

-----
Na, tazama, Kristo haonekani tena, unaona, tangu wakati huo pale . Lakini Yeye amepanda juu ya farasi mweupe. Kwa hiyo kama jamaa huyu amepanda farasi mweupe, yeye ni mwinga Kristo tu. Unaona? Mnalipata jambo hilo? Angalia, yule mpanda farasi aliye juu ya farasi mweupe hana jina lolote. Yeye aweza kutumia vyeo viwili au vitatu, unaona, bali yeye hana jina lolote. Lakini Kristo ana Jina! Ni lipi? Neno la Mungu. Hilo ndilo Jina Lake. “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu, naye Neno, alifanyika mwili.” Unaona?

Yule mpanda farasi hana jina, lakini Kristo anaitwa “Neno la Mungu.” Hivyo ndivyo Yeye alivyo. Yeye anaitwa hivyo. Sasa yeye ana Jina asilolijua mtu; lakini Yeye anaitwa, “Neno la Mungu.” Huyu jamaa haitwi chochote, mnaona, lakini yeye amepanda farasi mweupe. Mpanda farasi huyo hana mishale ya uta wake. Umegundua hilo? Alikuwa ana uta, lakini hakuna chochote kilichosemwa kuhusu kuwa na mishale yoyote, kwa hiyo lazima awe ni mlaghai. Vema. Huenda ana ngurumo nyingi sana, pasipo umeme. Lakini unaona ya kwamba, Kristo alikuwa na vyote viwili umeme na ngurumo, kwa kuwa kutoka katika kinywa Chake kunatoka Upanga mkali wenye makali kuwili, naye anawapiga mataifa kwa huo. Jamaa huyu hawezi kupiga chochote, unaona, bali yeye anatekeleza fungu la mnafiki. Yeye anaenda, amepanda farasi mweupe, akienda apate kushinda.

Kristo ana Upanga mkali, na, tazama, unatoka kinywani Mwake. Neno lililo hai, yaani, Neno la Mungu lililofunuliwa kwa watumishi Wake. Kama Yeye alivyomwambia Musa, “Nenda, simama pale, uishikilie fimbo hiyo huko; uite inzi,” na inzi wakatokea. Hakika. Lolote alilosema, Yeye alilitenda; nalo likatimia, Neno Lake lililo Hai. Mungu na Neno Lake ni Mtu yule yule. Mungu ni Neno. Ni nani huyu mpanda farasi wa siri wa wakati wa kwanza wa kanisa basi? Ni nani? Hebu na tuliwazie hilo. Ni nani huyu mpanda farasi wa siri anayeanzia ule wakati wa kwanza wa kanisa na kuendelea kumpanda mpaka kufikia Umilele, anaenda mpaka mwisho?

Muhuri wa Pili unatokea na kuendelea moja kwa moja mpaka mwisho. Muhuri wa Tatu unatokea na kuendelea mpaka mwisho. Wa Nne, wa Tano wa Sita, wa Saba, kila mmoja wa hiyo, unaishia hapa mwishoni. Na katika wakati wa mwisho, Magombo haya yaliyokunjwa wakati huu wote, yenye siri hizi ndani, yatavunjwa. Ndipo siri zitatokea, zijulikane kwamba ni nini. Lakini, kwa kweli, zilianzia katika ule wakati wa kwanza wa kanisa, kwa sababu kanisa, ule wakati wa kwanza wa kanisa, ulipokea Ujumbe kama Huu Huu.

“Mpanda farasi mweupe alitoka akaenda.” Mnaona? Yeye ni nani? Yeye ana nguvu katika nguvu zake za kushinda. Je, mnataka niwaambieni huyo ni nani? Huyo ni yule mpinga-Kristo. Ni yeye kabisa. Sasa, kwa sababu, mnaona, kama mpinga-Kristo, Yesu alisema, ya kwamba, “Hizo mbili zingefanana sana hata ingewapoteza walio wateule, (Bibiarusi) kama yamkini.” Mpinga-Kristo, ni roho wa mpinga-Kristo.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Muhuri Wa Kwanza.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Forerunner.

Jina la Mungu.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni apple?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

  Maandiko Anasema...

Kisha nikaona katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa muhuri saba.

Nikaona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kuu, N'nani astahiliye kukifungua kitabu, na kuzivunja muhuri zake?

Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama.

Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama.

Ufunuo wa Yohana 5:1-4


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDF Kiingereza)

Marriage and Divorce.

(PDF Kiingereza)

William Branham Life
Story.

(PDF Kiingereza)

How the Angel came
to me.
(PDF Kiingereza)


Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.