Unyakuo.

<< uliopita

ijayo >>

  Neno lililo hai mfululizo.

Unyakuo.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Unyakuo.

Zaburi 27:4-5,
4 Neno moja nimelitaka kwa BWANA, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa Bwana, Siku zote za maisha yangu, Niutazam uzuri wa BWANA, Na kutafakari hekaluni MWAKE.
5 Mradi atanisitiri bandarini MWAKE. Siku ya mabaya, Atanisitiri katika sitara ya hema yake, Na kuniinua juu ya mwamba.

Sasa, Mungu anayo njia ya kutenda mambo. Na Yeye habadilishi utaratibu Wake kamwe. Yeye huwa habadilishi uta... Yeye ni Mungu asiyebadilika. Katika Amosi 3:7, Yeye alisema, “Asingefanya jambo lolote duniani hadi kwanza awafunulie watumishi Wake hao manabii. “Na kama ilivyo hakika tu kwamba Yeye aliahidi hilo, Yeye atalifanya.

Sasa tumekuishapita vipindi saba vya kanisa. Lakini tumeahidiwa katika siku za mwisho, kufuatana na Malaki 4, kuwa kungekuweko na kurejea tena kwa nabii katika nchi. Hilo ni sahihi. Tazama asili yake, yeye angekuwa wa namna gani. Yeye daima... Mungu anaitumia roho hiyo mara tano: kwanza ndani ya Eliya ndani ya Elisha, katika Yohana Mbatizaji, kuliita kanisa litoke na mabaki ya Wayahudi. Mara tano “neema” Y-e-s-u, I-m-a-n-i na hivyo ni hesabu ya neema. Mnaona? Vyema.

Sasa, kumbuka, Ujumbe umeahidiwa. Na mafumbo haya yote yaliyokuwa yamefungwa matita matita na mafungamano ya kidini itahitaji - nabii moja kwa moja toka kwa Mungu afunue hili. Na hilo ndilo hasa yeye aliloahidi kufanya. Mnaona? Sasa kumbuka “Neno la Bwana huja kwa nabii,” siyo kwa Mwanatheolojia. Nabii ni picha ya Neno la Mungu katika kioo. Yeye hawezi kusema chochote; hawezi kusema mawazo yake mwenyewe. Yeye ataweza tu kusema kile ambacho Mungu hufunua. Hata kwa yule nabii Balaamu alipojaribiwa ili auzwe, auze haki yake, yeye alisema; “Nabii yoyote awezaje kusema chochote isipokuwa kile ambacho Mungu aweka kinywani mwake? Ni kitu ambacho huwezi kusema kitu kingine chochote. Na umezaliwa kuwa hivyo. Si zaidi ya ambavyo unge.

Kama ungeweza kusema, “Ni-ni-siwezi kufungua macho yangu,” wakati unatazama. Mnaona? Huwezi , huwezi kunyosha mkono wako, wakati unaweza. Mnaona? Huwezi ukawa mbwa wakati wewe u binadamu. Mnaona? Wewe umeumbwa tu uwe hivi. Na Mungu pia, kila wakati katika vipindi, kwa njia ya Isaya, Yeremia na wote, Eliya, katika vipindi vilivyopita. Wakati kikundi cha kidini kingefanya kila kitu kiwe vurugu, yeye angemtuma nabii, amwinue kutoka mahali pasipojulikana. Yeye hakuwa mmoja wa taratibu zao, na alinena Neno Lake. Waliitwa watoke kutoka maisha haya na wakawa wamekwenda kabisa, watu wa kweli ya Mungu tu, wasiokuwa na taratibu. Na daima hiyo ndiyo iliyokuwa njia ya kumtambua yeye. Yeye alisema, “Kama yupo mmoja miongoni mwenu aliye wa kiroho au nabii...”

Sasa, manabii. Kuna kitu kama, “ karama ya unabii” katika kanisa, lakini nabii amechaguliwa tangu asili na kuandaliwa kwa ajili ya saa atakayokuwepo. Unaona? Ndiyo, bwana. Sasa, kama unabii unatolewa, wawili au watatu sharti waketi na kuamua kama ulikuwa sahihi au la, kabla kanisa halijaupokea. Lakini hakuna yeyote aliyeketi mbele ya nabii, kwa sababu yeye alikuwa- alikuwa Neno la Mungu kamili. Alikuwa Neno katika siku yake. Ungemuona Mungu kama katika kioo amedhihirishwa. Sasa, Mungu ameahidi kututumia hilo tena katika siku za mwisho, ili kumtoa Bibi arusi nje ya vurugu ya kidini, katika njia pekee ambayo hili laweza kufanywa.

Haitawezekana kutendeka kamwe, Kanisa haliwezi kumpokea Kristo. Sisi Wapentekoste, hatuwezi kuubeba Ujumbe huu na kuendelea nao katika hali ambayo kanisa limo ndani yake leo. Tutawezaje kuendelea siku za mwisho katika hali ambayo wako ndani yake leo, wakati kila mmoja yuko kinyume cha mwenzake, na kila kitu kingine, na kidini? Aaa rehema ! Ni vurugu imeishia kwenye madhehebu. Na wakati wowote... Na wakati wowote.... Namwalika mwanahistoria yeyote ku-ku- kukosoa hili. Kila wakati ujumbe ulipopita duniani, na wakati walipouundia shirika la dini ulikufa pale pale. Na Upentekoste umefanya kitu kile kile ambacho hao wengine wote walifanya, huu Upentekoste uliokuwa umekuja huku nje.

Ninyi Assemblies of God, wakati Mababa zenu wa kale na mama zenu walipotoka nje ya hayo mashirika ya dini nyuma huko katika lile Baraza Kuu la zamani walipiga kelele na kumsifu Mungu, na walipinga yale mambo. Na mmegeuka kama mbwa kurudia matapishi yake na nguruwe kwenye matope yake” na mmefanya kitu kile kile wengine walichokifanya. Na sasa mmekuwa mno wa taratibu za kidini, na mmefunga mioyo yenu ya huruma. Yakupasa uwe na kadi ya ushirika kabla hujaruhusiwa angalau, kushirikiana nanyi.

Ninyi Oneness, Mungu aliwapa ujumbe kama huo, na badala ya ninyi kuendelea mbele, na kuwa tu wanyenyekevu, na kuendelea mbele, mlilegeza kamba na kujiunda kuwa shirika la dini la kikundi chenu. Sasa nyote mko wapi? Ndoo ile ile. Ndivyo hivyo kabisa. Na Roho wa Mungu akiendelea mbel. “Mimi Bwana nimepanda Hili, nitalinyeshea Hili, mchana na usiku. Wengine wasije... Yeye alipangilia kuwa mambo haya yawepo, na ni sharti atume Hili.

Jambo la kwanza linatokea, wakati anapoanza kushuka kutoka Mbinguni, kunakuwepo na mwaliko. Huo ni nini? Ni Ujumbe kuwakusanya watu pamoja. Ujumbe unatokea, kwanza, sasa, ni wakati wa kuzitengeneza taa, “Amkeni mzitengeneze taa zenu”. Hilo lilikuwa lindo la ngapi? La saba, sio la sita. La saba “Tazama, Bwana Arusi anakuja Amkeni na mzitengeneze taa zenu” Na walifanya hivyo. Baadhi yao walikuta hawana mafuta yoyote katika taa zao. Unaona? Lakini ni wakati wa kuzitengeneza taa. Ni wakati wa Malaki 4. Kile ambacho alia... Ni Luka 17. Ni-ni Isa... Huo unabii wote ambao, Hilo laweza kuweka katika mpangilio wake kikamilifu kwa ajili ya siku hii katika Maandiko, tunaliona hilo likiwa hai pale pale. Hakuna...

Angalia mambo haya yakitokea ndugu yangu, dada. Wakati, Mungu huko Mbinguni anajua ningeweza nikafia hapa jukwaani sasa hivi. Wewe-ilikubidi utembee tembee kwa kitambo. Ni kwamba tu.... Ni jambo kuu unapomwona Mungu amekuja kutoka Mbinguni, akasimama mbele ya vikundi vya watu, na akasimama pale na kujidhihirisha kama alivyowahi kufanya nyakati nyingine. Na hiyo ndiyo kweli, na Biblia hii ikiwa wazi unaona? Vema. Tupo hapa.

Ta utaratibu wa madhehebu umekufa. Haupo. Hautaamka tena kamwe. Utachomwa moto. Hicho ndicho unachofanya na makapi huko shambani. Kimbia kutoka huko. Ingia ndani ya Kristo, Usiseme, “Mimi ni wa Methodist, Mimi ni wa babtisti, Mimi ni wa pentekoste” ingia ndani ya Kristo. Kama wewe uko ndani ya Kristo, hakuna Neno lililoandikwa ndani Hapa usiloliamini. Sijali chochote ambacho mtu mwingine yeyote amesema. Na ndipo Mungu anafanya kitu hicho kudhihirisha. Sababu, wewe, wakati Yeye anapomwaga Roho juu ya Neno, kitu gani kinatokea? Kama tu kuweka maji juu ya mbegu nyingine yoyote. Itaishi na itazaa kwa namna yake... Unasema, “Mimi nina ubatizo wa Roho Mtakatifu.” Hivyo haimaanishi kuwa umeokoka, siyo hata kwa mbali.

Tazama hapa. Wewe u kiumbe wa utatu. Ndivyo ulivyo. Ndani katika jamaa huyu hapa pana nafsi, baada ya hapo roho, baada ya hapo mwili. Sasa una hisi tano katika mwili ili kuwasiliana na nyumbani kwako hapa duniani. Hizo haziwasiliani na vinginevyo isipokuwa hivyo. Unazo hisi tano za roho, hapa: upendo, dhamiri na kadhalika, za hiyo, Lakini ndani hapa ndimo unamoishi. Hicho ndicho wewe ulicho. Je, Yesu hakusema “Mvua huwanyeshea wenye haki na wasio haki? [Kkusanyiko linasema - “Amina” -Mh.] Uweke gugu nje hapa, na ngano nje pale, na umwagilie zote maji, na uwekee zote mbolea, na vitu kama hivyo, je vyote viwili havitaishi kwa maji yale yale? [“Amina”] Hakika. Vema, hicho ni kitu gani? Mojawapo itazaa gugu, kwa sababu hicho ndicho lilicho. Gugu litainua mikono juu na kupiga kelele vile vile kama ngano itakavyofanya.

Je, Biblia haisemi. “Katika siku za mwisho kutotokea Makristo wa uongo [Kusanyiko linasema, Amina”-Mh]. Siyo “Yesu wa uongo”, sasa. “Makristo wa uongo” watiwa mafuta, Wanaolijia Neno wakiwa watiwa mafuta wa uongo; waliotiwa mafuta ya kidhehebu, lakini siyo ili kulijia Neno. Kwani Neno litajishuhudia lenyewe. Halihitaji kitu kingine chochote. Litajishuhudia lenyewe. “Na watatokea watiwa mafuta wa uongo. “ Mnayo kanda yangu niliyohubiri juu ya hilo. Na yule mtiwa.... Aa, ungelimwita mmojawapo, useme. Aaa, wewe Yesu fulani?” “Aa, hakika, hapana”. Hawawezi kusimamia hilo.

Lakini inapofikia pale “Aa utukufu”! Ninao upako. Kumbuka Kayafa alikuwa nao, pia, na akatabiri. Lakini hilo halihusiani kwa chochote na hili, kwa ndani. Labda iwe kwamba huyo alikuwa mbegu ya Mungu, chembe kutoka mwanzo, Sijali unapiga kelele kiasi gani, unanena kwa lugha kiasi gani, unakimbia, unapiga kelele. Hilo halihusiani chochote na hili. Gugu laweza kuwa na hali zote mazao mengine yaliyo nayo. Mimi nimeona makafiri wakisimama, na kupiga makelele, na kunena kwa lugha nana kunywa damu toka kwenye fuvu la kichwa cha mwanadamu na kumwitia Shetani. Mnaona? Hivyo usii... Mojawapo ya hisia na vitu kama hivyo, sahau hilo. Ni moyo wako katika hilo Neno, na huo ni Kristo. Ilete ndani pale, na itazame ikijifanya yenyewe kufahamika, wakati inapofunguka tu kama mbegu nyingine yoyote, na kujitangaza yenyewe katika kipindi inachoishia ndani yake.

Luther hakuleta chochote isipokuwa kitawi. Hawa wengine waliweza hivi vitu vingine. Sasa tupo katika kipindi cha ngano. Akina Luther wa Luther ilibidi wamlete Luther halisi Pentekoste halisi ilipasa ilete pentekoste halisi. Ndivyo hivyo. Lakini tumekwisha pita kipindi hicho, na tunaendelea mbele. Unajua, kanisa Katoliki lilipoanza, lilikuwa la Upentekoste? Na kama kanisa la Pentekoste lingedumu kwa miaka elfu mbili lingekuwa katika hali mbaya kuliko Katoliki ilivyo sasa. Hivyo ndivyo hasa. Nawaambia hilo ndugu zangu, dada zangu, ambao ninawapenda. Na Mungu anajua hilo. Lakini kumbuka, marafiki, yanibidi kukutana nanyi ngambo ya pili penye Hukumu. Na hilo huenda lisichukue muda mrefu mno. Yanipasa niwe na ushuhuda wa kile kilicho Kweli.

Wakati nilipoingia katika mikutano pamoja nanyi, nikiwaombea wagonjwa, hilo lilikuwa jema. Lakini, wakati nijapo na Ujumbe! Kama Ujumbe wowote ukiwaandaa watu, ni Ujumbe wa kweli. Kama ni miujiza ya Mungu halisi, iliyo ya kweli, na ukaning’inia humo humo katika hilo shirika la dini, unajua hilo halitokani na Mungu, kwani hicho kitu tayari kimekwishatangazwa. Yesu alipita huko na kuponya wagonjwa, ili kudaka macho yao, hao watu, kisha Ujumbe Wake. Hilo ni sahihi. Lakini sharti uwe na kitu fulani ambacho Mungu anakwenda kutambulisha. Yeye tu... Uponyaji wa Kiungu, miujiza Yake namna hiyo, ili tu kudaka macho ya watu. Kusudi Lake kuu ni Ujumbe. Hicho ndicho, kile kinachotoka ndani hapa. Yeye anajaribu kupata kukubalika na watu, ili waketi na kumsikiliza Yeye, unaona, kwani wamo baadhi ndani pale waliokusudiwa Uzima. Baadhi ya nafaka, ngano, zilianguka ardhini, ndege wakazidonoa. Na nyingine zikaanguka kwenye miiba. Na baadhi zilikuwa, zilikwenda katika ardhi iliyoandaliwa, ardhi iliyoandaliwa kabla, na zikazaa.

Sasa,, jambo la kwanza, ni mazingira. Jambo la kwanza ni parapanda na... au sauti... Mwaliko. Na kisha sauti, na ndipo parapanda. Mwaliko: Mjumbe akiwaandaa watu wawe tayari. La pili ni sauti ya ufufuo: Sauti ile ile, ambayo sauti kuu katika Yohana Mtakatifu 11:38-44, ile iliyomwita Lazaro toka kaburini. Kumkusanya Bibi arusi pamoja; na ndipo ufufuo wa wafu, unaona, kudakwa pamoja Nalo. Sasa tazama mambo matatu yakitukia. Linalofuata ni nini? Ilikuwa ni parapanda. Sauti... Mwaliko, Sauti, parapanda.

Sasa, jambo la tatu ni parapanda ambayo, daima penye sikukuu ya mabaragumu, ni kuwaita watu waende karamuni. Na hiyo itakuwa ni karamu ya Bibi arusi, Karamu ya Mwanakondoo pamoja na Bibi arusi, angani. Mnaona? Jambo la kwanza linalotokea ni Ujumbe Wake, kuwakusanya Bibi arusi pamoja. Linalofuata ni ufufuo wa Bibi arusi aliyelala mauti, wale-wale waliokwishakufa, huko nyuma katika vipindi vingine, wote wanadakwa pamoja. Na parapanda, karamu huko Mbinguni, angani. Mbona, hicho ndicho kitu kitakachotukia, marafiki. Tupo pale, tayari sasa. Jambo moja pekee, Kanisa linalotoka nje, lapasa lilale mbele ya Mwana ili liive. Bado kitambo kidogo, ile tingatinga kuu itawasili. Ngano itateketezwa, yale mabua, lakini ngano itakusanywa kwenye ghala Yake. Mnaona?

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Unyakuo.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Forerunner.

Jina la Mungu.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni apple?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

   Maandiko Anasema...

Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.

Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.

Basi, farijianeni kwa maneno hayo.

1 Wathesalonike 4:16-18


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDF Kiingereza)
 

Maji katika Mwamba.

William Branham Life
Story.

(PDF Kiingereza)

How the Angel came
to me.
(PDF Kiingereza)

Pearry Green personal
testimony.

(PDF Kiingereza)

Marriage and Divorce.

(PDF)

As the Eagle
Stireth her nest.

(PDF Kiingereza)

Chapter 14
- Sabino Canyon

(PDF Kiingereza)


Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.